|
Zuberi
Amiri wa Yanga B, akichuana na Charles Domayo wa JKT Mgambo
*******************
Timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Yanga, imeifunga Mgambo JKT ya vijana pia, bao 1-0 katika mchezo wa utangulizi, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kabla ya kuanza kwa mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baina ya kaka zao, Yanga A dhidi ya Mgambo JKT ya Handeni, Tanga. Bao hilo pekee lilitiwa kimiani na Clever Charles dakika ya 65.
|
on Wednesday, October 31, 2012
Post a Comment