Katibu Tawala wa Manispaa ya Bukoba Clement
Ndiomukama, akimkabidhi kitita cha Tsh.900,000 Nahodha wa timu ya Kabanga
Bushasha, Eliudi Prospa baada ya kuibuka mabingwa kwenye mashindano ya
(Mitumbwi) Balimi Boat Race Wilayani Bukoba Mkoani Kagera jana
ambapo washiriki walishindana kuendesha mitumbwi kwa
makasia.
Mabingwa wa mashindano ya Mitumbwi ya Balimi
(Balimi Boat Race) Mkoani Kagera upande wa wanaume timu ya Kabanga
Bushasha wanaume wakishangilia mara baada ya kuwa mabingwa wa mkoa huo na
kukabidhiwa jumla ya shilingi laki tisa (900,000) kama zawadi ya ushindi wa
kwanza.
Mabingwa wa mashindano ya Mitumbwi ya Balimi
(Balimi Boat Race) Mkoa wa Kagera upande wa wanawake Timu ya Seleka kutoka
Musila, wakishangilia mara baada ya kuwa mabingwa wa mkoa huo na kukabidhiwa
jumla ya shilingi laki saba (700,000) kama zawadi ya ushindi wa
kwanza.
Katibu tawala wa Manispaa ya Bukoba Clement
Ndiamukama, akifungua mashindano ya Mitumbwi ya Balimi (Balimi Boat Race)
yaliyofanyika Wilayani Bukoba Mkoani Kagera ambapo zaaidi ya timu 50 zenye watu
watano kila timu zilishiriki, ambapo walishindana kupiga kasia kwa umbali wa
Kilometa 3 kwenda na kurudi, kushoto ni Meneja wa Mauzo wa Kanda ya Ziwa Endrew
Mbwambo na Afisa wa Sumatra Kapteni Alex Katama.
Meneja wa Bia ya Balimi Edith Bebwa(kulia)
akizungumza na washiriki wa mashindano ya Balimi Boat Race Wilayani Bukoba
Mkoani Kagera mara baada ya kumalizika kwa mashindano hayo ambapo timu tano
zitakwenda kuwakilisha mkoa huo kwenye fainali zitakazofanyika mkoani Mwanza
Disemba mwaka huu.
Waokoaji wakiwakoa wapiga kasia kinamama
ambao walipinduka
Mabingwa Wanaumr
Wakishangilia Baada Ya Kuwasili
*****************
WASHIRIKI wa shindano la mitumbwi ya Balimi
(Balimi Boat Race) ambayo ni maalum kwa mikoa ya kanda ya ziwa wametakiwa
kutumia pesa wanazozipata kwaajili ya kujiendeleza kwenye miradi ya
maendeleo.
Akizungumza mara baada ya mashindano hayo
Meneja wa Kinywaji hicho Cha Balimi Edith Bebwa, alisema lengo la mashindano
hayo ni kutoa shukrani na kuwawezesha wanywaji wake hivyo wanapaswa kuzitumia
kwenye kujiendeleza kwenye miradi yao.
“Nawaomba mlioshinda na washiriki wengine
ambao pia mmepata pesa hizo mzitumie kwenye miradi yenu kama ni mvuvi basi
ongeza chombo kingine au nyavu ili mradi uzitumie kwenye uzalishaji” alisema
Bebwa.
Awali akifungua mashindano hayo Katibu Tawala
wa Manispaa ya Bukoba Clement Ndiamukama aliwataka washiriki watakaoshinda
kutobweteka na ubingwa badalayake wajipange kwa mazoezi ili kwenye fainali ya
mashindano hayo waupe heshima Mkoa wa Kagera.
“Tunataka mtuletee heshima kwahiyo wale
watakaoshinda watambue wajibu huo wakuletea heshima Mkoa,” alisema
Ndiomukama.
Mashindano hayo ambayo yalianza Mkoani Kigoma
October 27 mwaka huu yanatarajiwa kumalizika kwenye fainali zitakazofanyika
mwezi Disemba mwaka huu Mkoani Mwanza.
Post a Comment