………………………………..
Makamu wa rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Mohamed Gharib Bilal anatarajiwa
Kufungua Kongamano la Kwanza Afrika kuhusu usimamizi wa Utalii Endelevu
katika Hifadhi za Taifa.
Akizungumza na vyombo vya habari
Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu alisema
kuwa Kongamano hilo linatarajiwa kuanza rasmi October 15-18 katika
ukumbi wa kimataifa wa Mikutano wa (AICC) uliopo jijini Arusha.
Bw. Nyalandu alisema kuwa
kongamano hilo lina lengo la Kubadilishana uzoefu kuhusu fursa,
changamoto, zilizopo katika uhifadhi katika kukuza uchumi.
Alisema kuwa Tanzania ina vivutio
vingi vya utalii kama mapori ya akiba,hifadhi za taifa ngorongoro na
hifadhi za asili za misitu, pia vivutio vya asili na kiutamaduni kama
michoro ya mapangoni iliyopo Kondoa Irangi,eneo la kihistori la olduvai
na nyayo za kale za laytoli zilizopo ngorongoro.
Aidha alisema kuwa sekta ya
utalii inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa vitanda ambapo alisema
kuwa kwa ujumla swala hilo ni changamoto kubwa ambapo serikali
imejipanga kukabiliana nalo ili kuhakikisha kuwa sekta ya utalii inakuwa
na kuongeza pato la taifa.
“Serikali inafanya kila ambalo
linawezekana ili kuweza ili tuweze kuhakikisha kuwa vitanda vinatosha
pamoja na miundo mbinu kuwa bora zaidi ili viweze kutosha wageni ikiwa
ni pamoja na kuwafikisha kwa urais zaidi.”alisema bw.Nyaladu
Pia alifafanua kuwa jumla ya
washiriki 412 wanategemewa kushiriki kutokanchi 40 za bara la afrika
wakiwemo mawaziri kumi na tatu ambapo amesema kuwa washiriki 242 ambapo
ni sawa na asilimia 59% watakuwa ni watanzania na asilimia 41% ni
wageni kutoka nchi mbalimbali za bara la afrika.
Alisema kuwa Kongamano hilo
limeandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa lenye makao makuu yake
nchini Hispania kwa kushirikiana na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Post a Comment