Wakiwa na uhakika wa kuweka kibindoni kiasi cha
£350million kwa mkataba wa miaka 7 wa udhamini wa jezi na kampuni ya General
Motors ambao umepangwa kuanza mwaka 2014, Manchester United wamenunua haki za
udhamini wa jezi zao za kufanyia mazoezi walizoziuza kwa kampuni ya DHL mwaka
2010. Dili hilo lilokuwa na thamani ya £40 million kwa miaka minne kwa kuweka tu
maandishi matatu tu ya DHL kwenye jezi zao za mazoezi - hiyo ikiwa ni fedha
nyingi kuliko wanazopata vilabu vingine kwa udhamini wa jezi zao rasmi za
mechi.
Lakini kutokana na tathmini yao, United wanaona fedha hizo ni kidogo kutokana na thamani yao kupanda, ukizingatia walikuwa wakipata kiasi cha £20 million kwa mwaka kwa udhamini wa AON lakini sasa wataanza kuvuta karibia £50 million kwa mwaka kutoka GM."Tumefanikiwa vizuri sana kukubaliana na kununua haki zetu za udhamini wa jezi za mazoezi kutoka DHL kuanzia mwakak 2013," klabu hiyo ilisema. "DHL wataendelea kuwa wadhamini wa masuala ya uchukuzi duniani kote.

"Masuala ya ukuaji wa thamani yetu yalikuwepo katika makubaliano ya mwanzo, ni ni kweli thamani yetu imepanda na mfano mzuri ni dili letu la hivi karibuni lilovunja rekodi lenye thamani ya $559 million la udhamini wa jezi na General Motors, hili linatufanya tuamini kutakuwepo na nafasi ya kuongeza thamani ya haki zetu za kibiashara."
Post a Comment