
Mh Balozi Kallaghe
Akisaini kitabu cha wageni

Mh Balozi akiongea na
wanajumuiya

Mh Balozi katika
akipokea zawadi kutoka kwa wanajumuiya

Ustadhi akiongea
machache wakati wa chakula

Mwenyekiti wa ZAWA
Hassan Khamis akimfafanulia jambo Mh Balozi

Watoto wa Kasida
wakisikiliza Hotuba ya Mh Balozi

Vijana wa Kasida
wakitumbuiza

Mh Balozi akionyeshwa
manzari tofuti ndani ya Jengo

Mh Balozi katika picha
ya pamoja
----
Salam,
Siku ya Jumamosi tarehe
27.10.12 Mh Balozi wetu wa Tanzania hapa nchini Uingereza alishiriki sherehe
ya siku kuu ya Iddi iliyofanyika London mashariki. Sherehe hii ya baraza la EID
(IDDI) iliandaliwa na Jumuiya ya East African Education Foundation
wakishirikiana na Jumuiya ya Wazanzibari waishio UK
(ZAWA)
Wakati akitoa hotuba
yake Mh Balozi Peter Kallaghe ambaye ndio aliekua mgeni rasmi siku hii ya leo,
alianza kwa kuwashukuru kwa mualiko huu mzuri alioupata na kuwatakia kila kheri
wale wote waliofanikiwa kutekeleza HIJA kwa mwaka huu 2012. Aidha Mh Balozi
ameahidi kuendeleza ushirikiano uliopo baina ya Ubalozi na Jumuiya mbalimbali za
Watanzania zilizopo nchini Uingereza na Ireland. Pia alivutiwa na kuipongeza
hatma ya East African Education Foundation kuazimia kununua Jengo hili kwa ajili
ya shughuli za kijamii na wanajumuiya wote kwa ujumla.
Baada ya kumaliza hotuba
yake Shekhe Nasssor Haroub nae aliongea na wanajumuiya akitilia mkazo zaidi
umuhimu wa Umoja na mshikamano kama Uislamu unavyo sisitiza kupitia Ibada ya
HIJA. Vilevile vijana wa kasida walipata fursa ya kutumbuiza alipomaliza kuongea
Shekhe Nassor.
Mwishoni Balozi alifanya
ziara fupi ya kukagua jengo hili na kupata maelezo kutoka kwa viongozi
mbalimbali wa Jumuiya ili kujua namna gani litakavyoweza kutumika mara baada ya
hatua za ununuzi zitakapo kamilika rasmi kwa gharama za paundi laki 6
(£600,000)
Asanteni,
Post a Comment