Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Mapato PPF yafikia bil. 91/-

MFUKO wa Pensheni (PPF) umefanikiwa kuongeza mapato yanayotokana na uwekezaji kutoka sh bilioni 43.45 mwaka 2010 hadi kufikia sh bilioni 91.38.
Hayo yalielezwa jana jijini hapa na Mwenyekiti wa bodi wa mfuko huo, Dk. Adolf Mkenda, alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa 22 wa mwaka wa wanachama na wadau wa mfuko huo.
Alisema mfuko huo umeendelea kufanya vizuri, kwani katika kipindi cha Januari mpaka Juni mwaka huu mapato yatokanayo na uwekezaji yamefikia sh bilioni 47.74 ambapo imevuka malengo waliyojiwekea ya kukusanya sh bilioni 47.71 katika kipindi hicho.
Mkenda alisema PPF iliongeza fedha zilizotumika kwenye uwekezaji wa vitega uchumi mbalimbali kutoka sh bilioni 672.2 mwaka 2010 hadi kufikia sh bilioni 837.6 mwaka 2011 ambapo mfuko huo unashiriki katika ujenzi wa vyuo vikuu kikiwemo cha Teknolojia ya Sayansi ya Kompyuta kilichopo Dodoma na cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela cha jijini hapa.
Alisema PPF imefanikiwa kupata tuzo tatu tofauti kutokana na kuendesha shughuli zake kwa uwazi kwa kuzingatia utawala bora ambapo moja walipewa na Chama cha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii cha Afrika Mashariki na Kati (ECASSA) na mbili kutoka Chama cha Kimataifa cha Hifadhi ya Jamii (ISSA).
Mwenyekiti huyo wa bodi alisema licha ya mafanikio waliyopata, lakini wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za uwekezaji na kiutendaji ikiwemo kubadilika kwa riba katika amana za uwekezaji, kiwango kikubwa cha mfumuko wa bei, ufinyu wa wigo wa uwekezaji, na uwasilishwaji wa fomu za madai kutoka kwa waajiri huku wakijua wazi kuwa waajiriwa wao bado wanaendelea na kazi.

CHANZO: TANZANIA DAIMA
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top