Afisa
Elimu Wilaya ya Mtwara Mwl.Mohamed Kahumbi,akionesha aina ya simu
iliyowekewa fedha katika akaunti ya M-pesa zinazotolewa bila malipo kwa
kwa akina mama wanaonyonyesha kuwawezesha kupokea fedha za kunulnuia
chakula chenye lishe kupitia mradi wa Lishe bora na salama wa shirika
la mpango wa chakula duniani – WFP. Mradi huo umezinduliwa juzi katika
kijiji cha Nanguruwe, Mkoani Mtwara.
Afisa
Elimu Wilaya ya Mtwara Mwl.Mohamed Kahumbi akimkabidhi simu ya mkononi
mmoja wa wanufaika wa mradi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani –
WFP wa kuwapatia fedha wanawake wanaonyonyesha na wajawazito fedha za
kununulia chakula chenye lishe kupitia M-pesa wakati wa uzinduzi
uliofanyika katika kijiji cah Nanguruwe mkoani Mtwara.
Mmoja
wa wanufaika wa mradi wa kuwawezesha wanawake wanaonyonyesha na
wajawazito mkoani Mtwara kupata chakula chenye lishe akiijaribu simu
aliyopatiwa ikiwa na fedha katika akaunti ya M-pesa atakazozitumia
kununulia chakula chenye lishe. Fedha na simu hizo hutolewa bila malipo
na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani – WFP kupitia mradi wake wa
Lishe bora na salama.
Akina
mama wa kijiji cah Nanguruwe mkaoni Mtwara ambao ni wanufaika wa mradi
wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani – WFP wa kuwapatia fedha
wanawake wanaonyonyesha na wajawazito fedha za kununulia chakula chenye
lishe wakijumuika na maofisa wa Vodacom kufurahia simu walizopatiwa
zikiwa zimeunganishwa na mtandao wa Vodacom kuwawezesha kupokea fedha za
mradi kwa njia ya M-pesa.
Post a Comment