Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni Mh.
Dkt. Getrude Rwakatare akitoa Ujumbe kwa Watanzania waliohudhiria Ibada Maalum
ya Kuliombea Taifa ambapo ametaka watu kutobaguana kwa misingi ya Dini, Ukabila
wala Siasa na kusema pamoja na Utawala bora pia tunahitaji maombezi ili tuweze
kufikia Malengo yaliyokusudiwa kulipeleka Taifa linapotakiwa
kufikia.
Dkt. Rwakatare amesema nia kubwa ya kufanya Ibada hiyo ya
Maombezi ni kutaka kuweka usawa kutokana na siku za hivi karibuni kuibuka kwa
Matamko mbalimbali kutoka kwa watu tofauti wakiwemo viongozi wa Kitaifa, Kidini
na wa baadhi ya Makundi yanayohitilafiana na kusema tukiomba kwa jina la Mungu
kila kitu kitakwenda kama tulivyomuomba ili Tanzania iendelee kuwa nchi ya Amani
na Utulivu kama ilivyokuwa miaka yote ambayo ni kimbilio la watu wa Mataifa
mbalimbali kwa sababu Watanzania hawajui kuchukiana na wamekuwa watu wa
kushikamana kwa miaka yote.
Post a Comment