***********
Na
Bin Zubeiry Blog
RAIS wa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Chillah Tenga amesema kwamba vita
dhidi ya rushwa katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ni ngumu na inahitaji
sapoti kubwa ya wadau na wapenzi wa mchezo wenyewe ili
kuifanikisha.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari leo, makao makuu ya TFF, Ilala mjini Dar es Salaam, Tenga
alisema kwamba pamoja awali kuwepo kwa mazingira ya ushahidi wa rushwa, lakini
wanashindwa kwa sababu wao wana mipaka yao.
“Hili la
rushwa kwa kweli ni gumu, ni gumu kwa sababu sisi tuna mipaka yetu, lazima
tupate ushirikiano na vyombo husika. Lazima tupate ushirikiano wa wapenzi
wenyewe wa mpira,”alisema Tenga.
Beki huyo wa
zamani wa kimataifa wa Tanzania, alisema wakati mwingine inakuwa vita hiyo
inakuwa ngumu zaidi anaposikia hata Waandishi wa Habari
wanahusika.
“Mimi
sijathibitisha, lakini watu wananiambia viongozi wenyewe wanashiriki mchezo huu.
Tena nasikia hadi nyinyi Waandishi wa Habari wakati mwingine mnatumiwa kupenyeza
rushwa, kwa kweli inasikitisha,”alisema Tenga.
Kuhusu
vipimo vya dawa za kulevya katika Ligi Kuu, Tenga alisema kwamba mchakato wa
zoezi hilo unaendelea na walichokifanya kwa sasa ni kuwataaribu na kuwapa muda
wahusika waache taratibu.
Alisema
wamewapa nusu msimu watumiaji wa mihadarati katika soka ya Tanzania kujiondoa
taratibu na tayari wamekwishawaambia hadi viongozi wa klabu zote, ili zoezi
hilo likianza liende vizuri.
“Hatutaki
kuwaadhiri vijana wetu, ndiyo maana tumewaambia mapema, ili wale ambao wanavuta
bangi kwa mfano, waanze taratibu kula chwingamu waache bangi, ili wakati
utakapofika, hakutokuwa na mzaha,”alisema Tenga.
Post a Comment