Ommy Dimpoz |
Nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini Ommy
Dimpoz amesema kuwa licha ya kutumia kiasi cha shilingi milioni 5 kurudisha
gari yake kwenye hali ya kawaida hawezi kumchukia msanii mwenzake Lord Eyez
anayeshikiliwa korokoroni hivi sasa kwa tuhuma za kuiba vifaa kutoka kwenye gari
yake.
“Nafahamu kuwa kuwa siruhusiwi kuzungumza lolote
kwa kuwa suala liko Polisi,ninachoweza kukwambia ni kuwa binafsi nimemsamehe
Lord na wenzake, sababu huwezi kujua kuhusu kesho, nimepanga kukutana naye na
kumwambia hili jambo, najisikia vibaya lakini nashukuru kuwa gari yangu
nimeshairekebisha na sasa ndiyo ninayoitumia tena licha ya kuwa nimetumiagharama
kubwa” alisema Dimpoz.
Post a Comment