Mbunge wa Arumeru
Mashariki (CHADEMA), Mh Joshua Nassari amekanusha taarifa zilizoandikwa na
magazeti ya Uhuru na Habari Leo kuwa jana alifyatua risasi na kuzua tafrani
katika uchaguzi wa kumtafuta Diwani wa Kata ya Daraja Mbili ya Jijini Arusha,
uchaguzi uliofanyika jana ambapo mgombea wa CHADEMA aliibuka
mshindi.
Nassari ameyasema hayo leo jioni wakati akihutubia katika
Mkutano wa hadhara kuzindua kampeni nyingine za chama chake kwa ajili ya chaguzi
za Serikali za Mitaa kwa ajili ya Halmashauri ndogo ya Mji wa Usa River
unaotarajiwa kufanyika Jumapili ijayo ya Novemba 4, 2012.
Mkutano huo
ambao umehudhuriwa na watu wengi, umefanyika katika viwanja vya Ngaresero
Usa-River ambapo mbali na Nassari, Katibu wa CHADEMA Kinondoni Ndg. Henry Kileo
nae alikuwepo na alipewa nafasi ya kuzungumza.
Nassari amedai kuwa katika
uchaguzi wa jana yeye alikuwa Wakala Mkuu wa CHADEMA Kata ya Bangata na hivyo
kumhusiha na ya Daraja Mbili haelewi inakujaje. Amedai kuwa mtu aliyefyatua
risasi ni Mwenyekiti wa UVCCM, Godwin Mwalusamba na kwamba Polisi walimuweka
ndani na kuandika maelezo yake, lakini anashangaa kuambiwa ni yeye wakati
siyo!
Akifafanua zaidi aliviomba vyombo vya usala avinavyohusika na
maswala ya vibali vya kumiliki silaha za moto, kufanya uchunguzi wao na waeleze
hiyo bunduki walimpa lini na ni risasi zimetumika, na kwamba kama ni kumkamata
yeye yupo huru muda wowote wanaweza kumkamata.
Loading...
BLOG RAFIKI
-
-
-
Alfajiri4 hours ago
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
-
Post a Comment