|
Aliyepata
kuwa mbunge maarufu kwa chama cha mapinduzi (CCM) wakati wa serikali ya Rais
Benjamin Mkapa na kuamua kukihama chama hicho na kujiunga na Chadema mwaka
2010 baada ya kuchakachuliwa matokeo yake Bw Thomas Nyimbo ameendelea
kufunguka zaidi baada ya kujiengua kuwa mlezi wa Chadema mikoa ya nyanda za
juu kusini ,
Nyimbo amesema serikali ya CCM inayumbishwa na
watendaji wake na kuwa Rais Jakaya Kikwete amekuwa akikwamishwa na wasaidizi
wake ambao ni mawaziri na manaibu waziri aliowateua
Akizungumza na
mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com wakati wa mahojiano maalum
yaliyofanyika Jijini Mbeya jana Nyimbo alisema kuwa CCM imeendelea
kuchukiwa kutokana na utendaji mbovu wa mawaziri na manaibu waziri na viongozi
wa kata ,wilaya na mikoa ambao baadhi wamegeuka kuwa mchwa na kufanya ufisadi
badala ya kusaidia wananchi wao.
Alitaja wizara ambazo mawaziri
wake wanafanya kazi nzuri katika kumsaidia Rais Jakaya Kikwete kuwa ni
pamoja na wizara ya ujenzi inayoongozwa na Dkt John Magufuli, wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inayoongozwa na waziri
Prof. Anna Tibaijuka, wizara ya
Uchukuzi inayoongozwa na Dkt. Harrison G. Mwakyembe,Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter
Muhongo, Waziri wa Maliasili na
Utalii Balozi Khamis Kagasheki
Aidha Nyimbo amempongeza waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera
na uratibu wa bunge Wiliam Lukuvi kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya na
kuwa iwapo nafasi hiyo angeteuliwa mtu asiyemchapakazi na makini nchi
yawezekana kabisa waziri serikali iliyopo madarakani ingekuwa imevunjwa
kutokana na mikikimikiki inayoendelea bungeni mjini Dodoma .
Hivyo Nyimbo alisema kuwa mawaziri na
manaibu mawaziri wanapaswa kufanya kazi hiyo kwa umakini zaidi ili
kuwatumikia wananchi bila kumuangusha Rais Kikwete
aliyewateua.
Wakati huo huo
Nyimbo alisema kuwa ipo haja ya Tanzania kuwa na sera ya nchi pamoja na kuwa na
wagombea binafsi wasiofungamana na vyama vya siasa ili kuwawezesha wagombea
hao kuwatumikia zaidi wananchi na Taifa badala ya kuvitumikia vyama vya
siasa ambavyo vyama vilivyovingi vimeanzishwa chumbani kwa kushauriana mume na
mke na baada ya hapo kuvisajili na kutafuta wafuasi zaidi . |
on Tuesday, October 30, 2012
Post a Comment