Meneja wa huduma za jamii wa Vodacom Foundation Mwamvua
Mlangwa, akikabidhi mfano wa hundi ya fedha kiasi cha shilingi Milioni 20, kwa
Mkurugenzi wa kituo cha Tanzania Mitindo House, Khadija Mwanamboka, Kwa ajili ya
kuanzisha chuo cha mafunzo ya Mitindo kwa Watoto yatima.
---
Dar es
Salaam, Zaidi ya watoto yatima 50 waishio katika
mazingira magumu watapata mafunzo ya ubunifu wa mavazi. Hii inafuatia kuanzikwa
kwa kwa kituo cha ubunifu wa mavazi , (Mitindo House) kitakachokuwa chini ya
Mwanamitindo maarufu, Hadija Mwanamboka.
Kituo hicho kitatoa
mafunzo ya ushonaji, ubunifu wa mavazi, na utengenezaji wa vito mbalimbali
kimefadhiliwa na mfuko wa huduma za jamii wa Vodacom (Vodacom
Foundation)
Akizungumza baada ya
kupokea mfano wa hundi ya shilingi Milioni Ishirini, Mkurugenzi wa kituo hicho,
Hadija Mwanamboka, amesema kuwa lengo lao ni kuwawezesha watoto yatima waishio
katika mazingira magumu na wasio na elimu kuweza kujitegemea kwa kujiajiri
wenyewe kutokana na ujuzi watakao upata.
“Tutatoa mafunzo kwa
watoto wanaoishi katika vituo mbalimbali vya kulelea watoto yatima, yatakayo
wawezesha kupata fursa ya kuonyesha vipaji vyao katika majukwaa ya sanaa na
baadae kuwawezesha kujiajiri wao wenywe.”
“Mafunzo haya yatatolewa
kwa mwaka mzima, wanafunzi ishirini na tano watapata mafunzo ya ushonaji na
ubunifu wa mavazi na wengine 25 watapata mafuzno ya uchongaji wa vito mbalimbali
na uchoraji,” alisema Hadija.
Kwa
upande wake, Meneja wa Huduma za jamii wa Vodacom Foundation, Mwamvua Mlangwa
amesema kuwa Vodacom Foundation imedhamiria kuboresha maisha ya jamii ya
watanzania wanaoishi katika mazingira magumu.
“Vodacom Foundation
itaendelea kuwaunga mkono watanzania hususani wale wanaoishi katika mazingira
magumu kwa kuwasaidia kujenga maisha yao na kusaidia kukua kwa uchumi wa nchi
kupitia mipango mbalimbali tuliyonayo katika kitengo chetu,” alisema
Mlangwa.
Kuhusu Vodacom
Tanzania:
Kampuni ya Vodacom
Tanzania Limited ina dhamira ya dhati ya kushirikiana na jamii katika shughuli
za maendeleo kupitia taasisi yake ya Vodacom Foundation. Vodacom Foundation ina
nguzo kuu tatu: Afya, Elimu na Ustawi wa Jamii. Hadi sasa taasisi hiyo
imechangia zaidi ya miradi 120 ya kijamii nchini. Aidha, imeshinda tuzo
mbalimbali za kitaifa na za kimataifa katika nyanja ya Uwajibikaji wa Mashirika
kwa Jamii. Hizi ni pamoja na East African CSR Awards na Diversion and Inclusion
Award ambayo hutolewa na kampuni mama ya Vodafone .
Vodacom Tanzania Limited
ni kampuni ya simu za mikononi inayoongoza Tanzania inayotumia teknolojia ya
kisasa ya mawasiliano. Vodacom Tanzania ni kampuni tanzu ya Vodacom Group (Pty)
Limited, South Afritca, ambayo pia ni kampuni tanzu ya Vodafone Group UK.
Vodacom Group (Pty) Limited inamiliki hisa ailimia 65 Vodacom Tanzania na
asilimia 35 zilizobaki zinammilikiwa na Mirambo Ltd.
Vodacom Tanzania
imetangazwa kuwa Super Brand (Chapa Bora Zaidi) kwa miaka mitatu mfululizo,
kutoka 2009 -2011.
Mwisho
Post a Comment