Balozi wa Tanzania
nchini Uingereza, Mhe. Peter A. Kallaghe, jana amemvisha rasmi cheo kipya
Mwambata wa Jeshi, Brigadia Jenerali Pelegreen Mrope kwa niaba ya Mheshimiwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, katika
hafla fupi uliyofanyika Ubalozini hapo,Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania alimtunukia cheo hicho kipya aliyekuwa Kanali Mrope tarehe 17
Septemba 2012. Pichani wakishuhudia shughuli hiyo ni Naibu Balozi, Mhe. Chabaka
Kilumanga na Dada Emmy Massaba, Katibu Mahsusi wa Brigadia Jenerali
Mrope.
Mheshimiwa
Balozi, Peter Kallaghe, akiwa kwenye picha ya pamoja na Brigadia Jenerali
Pelegreen Mrope, (kulia) na Naibu Balozi, Mheshimiwa Chabaka Kilumanga mara
baada ya kumvishwa cheo chake kipya jana mchana.Picha na Habari Rashid
Dilunga Ubalozi
wa Tanzania Nchini Uingereza
Post a Comment