Msanii
wa kundi la WEUSI Lord Eyez alifikishwa katika mahakama ya wilaya ya Kinondoni
jijini Dar es salaam leo asubuhi akitokea mahabusu katika kituo cha polisi
Oysterbay
Msanii huyo pamoja na kufika Mahakamani hapo alishindwa kupanda kizimbani baada ya hati ya mashitaka kutokidhi mahitaji ya kisheria.
Lord Eyez alifikishwa mahakamani hapo majira ya saa 3 asubuhi akiwa kapakia gari ya Polisi aina ya defender, chini ya ulinzi mkali wa polisi na kupelekwa moja kwa moja mahabusu alikofichwa ili asionekane hadharani kwa waandishi wa habari ambao walijazana Mahakamani hapo.
Waaandishi wa habari hao pamoja na umati uliohudhuria Mahakamani hapo uliishiwa nguvu baada ya kupata taarifa kuwa Lord Eys hatapandishwa Kizimbani kwa sababu hati yake ya mashitaka ilikuwa na makosa tofauti na anayotuhumiwa nayo.
Chanzo chetu kilitujuza uwepo wa ulinzi mkali
kiasi cha kushindwa kuchukua picha ya aina yoyote iliyomuhusisha msanii huyo.
Post a Comment