Mgeni
Rasmi katika Mkutano wa 22 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau wa PPF,Naibu
Waziri wa Fedha,Mh. Saada Mkuya Salim akitoa hotuba yake wakati
akifungua mkutano huo unaofanyika leo kwenye ukumbi wa Kimataifa wa
Mikutano wa AICC,jijini Arusha.
Waziri
wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka akizunguza machache na Wanachana
na Wadau PPF wanaoshiriki kwenye Mkutano huo unaofanyika kwenye Ukumbi
wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC,jijini Arusha leo hii.
Mkuu wa
Mkoa wa Arusha,Mh. Magesa Mulongo akitoa salamu zake na kuwakaribisha
Wanachana na Wadau wote wa PPF waliofika kwenye Mkutano huo na kutaka
kutokuwa na mashaka yeyote kwani kila kitu kinakwenda sawa kabisa chini
ya uongozi wake.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wadhamini wa PPF,Dk. Adolf Mkenda akitoa hotuba yake mapema
leo asubuhi wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 22 wa Mwaka wa Wanachana na
Wadau PPF unaofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa
AICC,jijini Arusha.
Mkurugenzi
Mkuu wa PPF,William Eriyo akizungumza machache na kutoa utambulisho wa
baadhi ya viongozi wakuu wa PPF wakati wa Mkutano wa 22 wa Mwaka wa
Wanachana na Wadau unaofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa
AICC,Jijini Arusha leo.
Mgeni
Rasmi katika Mkutano wa 22 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau wa PPF,Naibu
Waziri wa Fedha,Mh. Saada Mkuya Salim akikabidhi tuzo na Cheti cha
ushindi kwa Meneja wa Fidia na Faida wa Benki ya CRDB,Anamen Shangali
Mosha baada ya Benki hiyo kushika nafasi ya Pili kwenye Kipengele cha
Sekta ya Fedha.
Mgeni
Rasmi katika Mkutano wa 22 wa Mwaka wa Wanachana na Wadau wa PPF,Naibu
Waziri wa Fedha,Mh. Saada Mkuya Salim akimabidhi tuzo kwa Mkurugenzi wa
Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania,Julius Angelo (pili kulia).Benki Kuu ndio
walioibuka washindi wa Jumla wa tuzo hizo.
Wafanyakazi wa Benki Kuu wakiwa kwenye Picha cha Pamoja na Uongozi mzima ulopo meza kuu.
Wadau wakiwa kwenye Mkutano huo.
Post a Comment