|
Waziri Mkuu Mstaafu na
Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina Lowassa
wakiwa kenye picha ya pamoja na Warembo wanaowania Taji la Miss Tanzania
2012 pamoja na Viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania. | | |
|
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa
Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimia na Msimamizi (Matron) wa warembo
wa Miss Tanzania 2012, Irene Karugaba wakati warembo hao walipotembelea
Nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Monduli.
|
|
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa
Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akizungumza na Warembo wanaowania
Taji la Miss Tanzania 2012 waliofika nyumbani kwake Monduli leo na
kupata wasaa
kwa kuzungumza nae mambo mawili matatu juu ya mafanikio ya Mashindano
hayo na
Maendeleo ya Taifa letu kwa ujumla.
|
|
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa
Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akizungumza na Warembo wanaowania
Taji la Miss Tanzania 2012 waliofika nyumbani kwake Monduli leo na
kupata wasaa
kwa kuzungumza nae mambo mawili matatu juu ya mafanikio ya Mashindano
hayo na
Maendeleo ya Taifa letu kwa ujumla.
Waziri
Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowasa akisalimiana na Mrembo wa mkoa
wa Rukwa ambaye anaiwakilisha kanda ya Kaskazini, Vency Edward. Warembo
wanaowania taji la Redds Miss Tanzania 2012
walimtembelea nyumbani kwake eneo la Ngarash mjini Monduli, mkoani
Arusha.
*****************
WAZIRI
Mkuu Mstaafu wa Tanzania, na Mbunge wa Monduli, Edward Lowasa amewataka warembo
wanaoshiriki mashindano ya urembo ya Redds Miss Tanzania 2012 kutumia nafasi
hiyo waliyopata kutengeneza ajira kwao na vijana wenzao.
Lowasa
ameyasema leo wakati warembo wanaowania taji hilo walipomtembelea nyumbani
kwake eneo la Ngarash mjini Monduli na kuzungumza nao juu ya mambo mbalimbali
ya kisiasa, uchumi, utalii na sanaa ya urembo.
“ninyi
ni vijana, mnanguvu na hakika mkiyatumia vyema mashindano haya kwa malemngo
yanayostahili mnaweza kufika mbali kimaisha kwa kuwa wabunifu wa vitu
mbalimbali vya kufanya katika jamii na kujipatia ajira yenu binafsi na hata
kuajiri watu wengine,”alisema Lowasa.
Lowasa
ambaye amekuwa mstari wa mbele nchini katika kuhakiskisha vijana wengi wanapata
ajira nchini amesema sanaa ya urembo ikitumika vyema inamanufaa katika jamii na
ikitumiwa vibaya italeta matatizo na kuonekana sio kitu cha muhimu.
Akitolea
mfano wa Washindi wa Taji la Miss Tanzania waliopita hasa Hoyce Temu ambaye ni
Miss Tanzania 1999 kwa jinsi alivyo kuwa
mbunifu na kipindi chake cha Mimi na Tanzania ambacho mbali na kutoa fursa ya
kuweza kuibua matukio na maisha ya hali tofauti ya Watanzania lakini pia ametoa
ajira kwa wote anaofanya nao kazi.
Akizungumzia
juu ya ziara hiyo ya warembo hao ya kutembelea Vivutio vya Utalii nchini hasa
katuka Mikoa ya Kanda ya Kaskazini amesema kuwa ni jambo jema hasa kuziangatia
kuwa utangazaji wa vivutio vya utalii vya nchi yetu upo chini hivyo warembo
watasaidia jamii kuelewa na kujenga utamaduni wa kuitembelea vivutio vya utalii
na kuhamasisha utalii wa ndani.
Kuhusiana
na hali ya kisiasa nchini Lowasa amewaambia warembo hao kuwa Tanzania ipo
katika hali nzuri ya kisiasa jambo ambalo linazidi kuchochea maendelea na
kuleta umoja wa kitaifa ambao unawawezesha watu kuishi kwa amani.
“Siasa
yetu ni safi na kiukweli Serikali ya CCM inazidi kuidumisha hali ya amani
nchini jambo ambalo linawezesha hata ninyi kutembea bila matatizo kutoka sehemu
moja hadi nyingine, alisema Lowasa.
Pia
Lowasa aliipongeza Kamati ya Miss Tanzania chini ya Mkurugenzi wakew Hashim
Lundenga kwa kazi kubwa ya kuandaa mashindano hayo makubwa nchini ambayo
yamekuwa yalityoa ajira mbalimbali kwa washiriki wake na fursa za elimu.
Warembo wanaowania taji la Redds Miss Tanzania wapo
katika ziara ya kutembelea vivutio vya utalii Kanda ya Kaskazini pamoja na
kufanya shughuli za kijamii ikiwa ni pamoja na kuchangia watoto yatima na
waishio katika mazingira magumu.
|
on Wednesday, October 10, 2012
Post a Comment