Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MREFA YALIA NA MASHABIKI WA MBEYA

By Baraka Mpenja, Mbeya
****************
Chama cha soka mkoani mbeya MREFA kimelia na kasumba ya mshabiki mkoani hapa kususia mechi zinazohusisha timu ndogogo ligi kuu Tanzania bara na kuchagua mechi kubwa zinazohusisha vigogo vya soka la bongo.
Katika mahojiano maalumu na mweneyekiti wa MREA John Mwamwaja amesema ni tabia mbaya katika mchezo wa soka kuchagua mechi za kuangalia ukiwa shabiki wa soka.
“Unaweza kudharau mechi ya Prisons na Coastal ukisubiri ya Prisons na Simba, lakini mpira unaohusisha timu zisizo na majina unakuwa mzuri ukilinganisha na timu kubwa ambazo hukamiana sana na kuondoa ladha ya soka“. Mwamwaja amesema.
Mwenyekiti huyo wa MREFA amesema hayo kufuatia mashabiki wachache kujitokeza kuangalia mechi iliyopita wakati Prisons walipepetana na Oljoro JKT i kasumba mbaya katika soka .
Mwamwaja amewataka mashabiki mkoani hapa kujitokeza kila mechi kuangalia timu yao ili kuihamasisha msimu huu wa ligi.
Pia amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi katika mechi ya kesho wakati maafande wa Prisons watakapokabiliana na Azam FC katika dimba la kumbukumbu ya Edward Moringe sokoine mkoani Mbeya.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top