Kamati
ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilikutana Oktoba 11,
2012 kujadili michakato ya chaguzi mbalimbali za wanachama wa Shirikisho. Katika
kikao chake, Kamati ilijadili michakato ya chaguzi za viongozi wa Chama cha
Mpira wa Miguu cha Mkoa wa Rukwa (RUREFA), Chama cha Waamuzi wa Mpira wa Miguu
(FRAT), Chama cha Mpira wa Miguu cha Mkoa wa Shinyanga (SHIREFA) na Chama cha
Mpira wa Miguu cha Mkoa wa Dar es salaam (DRFA),.
Pia
Kamati ilijadili mchakato wa chaguzi za Chama cha Madaktari wa Michezo (TASMA)
na kupokea mchakato wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Mkoa wa Mbeya
(MRFA).
Baada
ya kujadili chaguzi hizo kwa kina, Kamati ilifikia uamuzi
ufuatao:
1. FRAT
Uchaguzi
wa FRAT haukufanyika baada ya wajumbe kugoma wakipinga kuondolewa kwa baadhi ya
wagombea. Kamati ilikubaliana kuiagiza Kamati ya Uchaguzi ya FRAT kuhakikisha
uchaguzi unafanyika Novemba 17, 2012 na kufanya maandalizi yote muhimu ikiwa ni
pamoja na sehemu ambako uchaguzi huo utafanyika. Mkutano utatakiwa kuwapigia
kura wajumbe waliopitishwa kugombea uongozi tu.
2. RUREFA
Baada
ya kufuta uchaguzi wa viongozi wa RUREFA na kuivunja Kamati ya Uchaguzi ya
RUREFA, Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeitaka Kamati ya Utendaji ya RUREFA kuteua
kamati mpya ya uchaguzi ya chama hicho kabla ya Oktoba 20, 2012 na kuiagiza
kamati mpya kuwa imeshatangaza mchakato wa uchaguzi ifikapo Oktoba 24,
2012.
3. SHIREFA
Kamati
ilipokea pingamizi dhidi ya baadhi ya wagombea uongozi wa SHIREFA na hivyo
kuagiza walioweka pingamizi na waliowekewa pingamizi pamoja na mwakilishi wa
Kamati ya Uchaguzi ya SHIREFA kuhudhuria kikao cha Kamati ya Uchaguzi ya TFF
kitakachofanyika Alhamisi ya Oktoba 18, 2012 kwa ajili ya maamuzi ya
mwisho.
4. MRFA
Kamati
ilipokea rufaa na pingamizi kutoka kwa baadhi ya wagombea walioenguliwa kuwania
uongozi wa chama hicho na hivyo imewataka walioweka pingamizi na waliokata rufaa
kuhudhuria kikao cha Kamati ya Uchaguzi ya TFF kitakachofanyika Oktoba 18, 2012
jijini Dar es salaam.
5. TASMA
Kamati
iliona mapungufu katika mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa TASMA na kuamua
chama hicho kifanye uchaguzi ifikapo Desemba mosi badala ya uchaguzi
kufanyika Oktoba 27, 2012 kama ilivyokuwa
imepangwa awali. Kamati ya Uchaguzi ya TFF inaiagiza Kamati ya Uchaguzi ya TASMA
kuhakikisha kasoro zilizojitokeza zinarekebishwa ili uchaguzi ufanyike kwa
mujibu wa Katiba ya chama hicho na Kanuni za Uchaguzi.
6. DRFA
Awali,
Kamati ya Uchaguzi ya TFF ilitangaza kuwa hatma ya uchaguzi wa DRFA itajulikana
baada ya kikao cha leo, lakini kutokana na wajumbe kutoweza kuhudhuria kwa
sababu tofauti, mustakabali wa suala hilo sasa utajulikana baada ya kikao cha
Oktoba 18, 2012.
Wagombea
na wadau wanaotakiwa kuhudhuria kikao cha Oktoba 18, 2012 wanataarifiwa kuwa
kikao hicho kitafanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi za TFF kuanzia saa
08:2012.
Kamati
inawaomba wajumbe wote kuhudhuria bila ya kukosa.
Post a Comment