Mgeni rasmi ambaye ni
Mratibu wa Tiba wa Manispaa ya Kinondoni, Sirila Mwanisi akizungumza katika
maadhimisha ya Siku ya Kunawa mikono katika viwanja vya Posta, Kijitonyama,
inayofanyika Oktoba 15, huku kwa wanafunzi hao wakiadhimisha jana katika viwanja
hivyo.
Wanafunzi ya 300 kutoka
shule za Msingi Shikilango, Kijitonyama Kisiwani, Mapambano, Mwangaza na Mwenge
wakionyesha mfano wa kunawa mikono mara baada ya kupewa
somo.
Wanafunzi wakitoa show mara
baada ya somo kuwakoloea.
Mwanafunzi wa shule ya
Mwenge akimuonyesha mwalimu wake (aliyeshika jagi) namna alivyofundishwa kunawa
mikono.
Mwanafunzi akiwadhibitishia
somo limeingia waalimu wake ambao wao walichukua jukumu la kummwagilia
maji.
Somo la kunawa mikono
likiendelea kudhibitishwa kwa vitendo na mwanafunzi wa shule ya msingi
Mapambano.
Walimu wakuwa na baadhi na
wanafunzi wa shule nne za msingi zilizohudhuria maadhimisho
hayo.
---
Na Mwandishi Wetu, Dar es
Salaam
WANAFUNZI zaidi ya 300
kutoka shule nne za jijini Dar es Salaam, jana ziliadhimisha Siku ya Kunawa
mikono katika viwanja vya Posta, Kijitonyama, inayofanyika Oktoba 15, huku kwa
wanafunzi hao wakiadhimisha jana katika viwanja hivyo.
Wanafunzi hao walikutana
katika viwanja hivyo kuanzia saa nne za asubuhi, huku mgeni rasmi akiwa ni
Mratibu wa Tiba wa Manispaa ya Kinondoni, Sirila Mwanisi.
Katika maadhimisho hayo,
wanafunzi hao walifundishwa jinsi ya kukabiriana na uchafu wakati wote, sambamba
na unawaji wa mikono kabla na baada ya kula.
Akizungumza katika viwanja
hivyo jana, Sirila alisema kwamba ni vyema watu wakajenga utamaduni wa kujitunza
kwa nyakati zote, ili wakabiriane ba maradhi yanayoweza kuepukika, vikiwano
vijidudu vinavyosababisha magonjwa ya tumbo na kipindupindu.
Alisema kwamba watoto
wadogo ndio wapo kwenye hatari zaidi, hivyo ni lazima wazazi na walezi pamoja na
jamii husika kuwaelimisha kwa ajili ya kuwaweka katika mazingira
mazuri.
“Watoto lazima waelimishwe
namna ya kunawa mikono kabla na baada ya kula, maana ndio nafasi ya kukabiri
vijidudu vya aina mbalimbali, ukiwamo ugonjwa wa kipindipindu ambao ndio hatari
zaidi ndani na na baadhi ya nchi za Afrika.
“Serikali kwa kushirikiana
na asasi mbalimbali tunaamini tutafanikisha usafi wa unawaji wa mikono kwa ajili
ya afya njema, ukizingatia kwamba ndio njia ya kufanikisha maisha bora kwa namna
moja ama nyingine, hasa wote tukiwa na afya njema,” alisema
Sirila.
Maadhimisho hayo ya siku ya
kunawa yameandaliwa na Kampuni ya PCB WITNA na kudhaminiwa na sabuni ya Protex
kwa ajili ya kukutanisha wanafunzi wa shule za Msingi Shikilango, Kijitonyama
Kisiwani, Mapambano, Mwangaza na Mwenge.
Post a Comment