Senegal imetupwa nje ya
kinyang’anyiro cha kuwania kombe la taifa bingwa barani Afrika
Tangazo hilo, linajiri
baada ya shirikisho la soka barani humo kuipa ushindi wa mabao mawili Ivory
Coast kufuatia vurugu za siku ya Jumamosi zilizosababishwa na mashabiki wa
Senegal
Vurugu hizo
zilisababisha kufutiliwa mbali kwa mechi kati ya nchi hizo mbili wakati Ivory
Coast ikiwa na mabao mawili bila dhidi ya Senegal katika uwanja wa
Dakaar.
Ivory Coast sasa
itashiriki katika michuano ya kuwania kombe hilo itakayofanyika nchini Afrika
Kusini mwezi Januari
Post a Comment