MSANII ndani ya tasnia ya filamu na tamthilia za kibongo Rayuu, azidi kujichora tattoo kwenye mwili wake ambapo sasa aamua kuchora kiunoni na sehemu nyingine nyeti.
Rayuu alisema
kuwa amechora michoro hiyo sehemu nyingi za mwili wake kuanzia kiunoni,
shingoni, kwenye maziwa, makalio na mapaja na alidai kuwa anajisikia
furaha kuwa na tattoo hizo kwani hajafanya kwa kushawishiwa na mtu.
Alidai kuwa hata hivyo kati ya michoro hiyo aliouweka kiunoni unasomeka jina lake la ‘Rayuu’ na mengine ni ya aina mbalimbali, “tattoo nazipenda sana lakini kati ya zote hii ya kiunoni naipenda kuliko zote ingawa aliyenichora aliikosea kidogo,” alisema.

Msanii huyo amecheza filamu kama ‘The Image’, ‘Trinita Show’, ‘Sound of Death’, ‘One House’, ‘Katikati ya Sherehe’ pamoja wasanii kibao maarufu, pia bado anaendelea kufanya vizuri kupitia tamthilia ya ‘Red Apple’ na ‘Millosis’.
Post a Comment