Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MTOTO WA SCHMEICHEL KUPATA SHAVU REAL MADRID



KASPER SCHMEICHEL

Mtoto wa Golikipa wa zamani wa manchester united peter schmeichel aitwaye Kasper schmeichel yuko mbioni kujiunga na klabu ya real madrid ya nchini hispania.

Mchezaji huyo ambaye anakipiga katika klabu ya leceister city ameonekana kuwastua watu wengi kutokana na kuhitajiwa na klabu ya real madrid.

Golikipa huyo anaonekana kuwa ni mbadala wa kudumu wa kipa namba moja wa real madrid iker casilas.

Taarifa hiyo imekuja muda mfupi baada ya kocha mkuu wa real madrid jose mourinho kutoa maagizo kwa kocha wa makipa wa real madrid Silvino Louro aweze kutafuta kipa ambaye anaweza kutoa changamoto kwa iker casilas liliripoti gazeti la Daily star, real madrid pia inawatupia macho wachezaji wawili roberto mwenye umri wa miaka 26 anayechezea zaragoza na Andres fernandez mwenye miaka 25 anayechezea osasuna.

Schmeichel 25 ambaye alianzia soka katika klabu ya manchester city kisha kuhamia Darlington(2006) na baadaye Notts Country alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa msimu wa Leceister.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top