Mtuhumiwa Pacficus
akipelekwqa mahakamani chini ya ulinzi mkali
Mtuhumiwa wa mauaji ya
aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten Daud
Mwangosi leo amefikishwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi ya Wilaya
kujibu shitaka lilalomkabili.Huku akiwa chini ya ulinzi mkali wa
askari.
Akisomewa shitaka lake
na mwendesha mashtaka wa serikali Mkuu lilian Ngilangwa , amesema mtuhumiwa huyo
ambaye ni askari mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23) mkazi wa FFU
Iringa, anakabiliwa na shitakala la mauaji ya makusudi.
Amesema mtuhumiwa huyo
mnamo 02 Septemba mwaka huu katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa
Iringa alimuua Daudi Mwangosi kwa makusudi kinyume na kifungu cha sheria namba
148 kifungu kidogo 5A.i cha makosa ya jinai.
Mbele ya Hakimu Mkuu Mwandamizi wa mahakama ya hakimu Mfawidhi ya Wilaya Dyness Lyimo mtuhumumiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haiwezi kusikiliza kesi za mauaji.
Kwa mujibu wa kesi za
jinai, sheria kifungu 196 kanuni ya adhabu Cap. 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka
2002, kinakataza mtuhumiwa wa mauaji ya kukusudia kupewa
dhamana.
Mtuhumiwa amerudishwa
mahabusu kutokana na kesi yake kukosa dhamana kisheria na kesi hiyo imeahirishwa
hadi 7 Novemba mwaka huu itakapotajwa tena mahakamani
hapo.
Mtuhumiwa huyo aliletwa
chini ya ulinzi mkali wa polisi kaitka gari la polisi lenye number za usajili PT
1467.
Huku waandishi wa habari
wakizuiwa kupiga picha jambo lililosababishwa kusukumwa kwa mwandishi wa majira
Elias Ally na mmoja wa Polisi hao.


Post a Comment