*YATAFANYIKA TAREHE
24-28 OKTOBA, 2012 JIJINI JOHANNESBURG, AFRIKA
KUSINI
*KUSHIRIKISHA WABUNIFU
ZAIDI YA 35 AFRIKA, NI MSHIRIKI PEKEE KUTOKA TANZANIA.
Mbunifu maarufu wa mavazi
kutoka Tanzania, Mustafa Hassanali ndiye Mtanzania pekee katika fani ya mitindo
aliyepewa mualiko wa kushiriki katika maonyesho ya Wiki ya Mitindo Afrika chini
ya African Fashion International (AFI) yatakayofanyika kwa siku nne kuanzia
tarehe 24-28 Oktoba, 2012 katika ukumbi wa Melrose Arch, jijini Johannesburg,
Afrika ya Kusini.
Mashindano hayo
yanayodhaminiwa na kampuni ya kutengeneza Magari ya Mercedes-Benz yanatarajiwa
kuwashirikisha wabunifu wa mavazi zaidi ya 35 kutoka sehemu mbalimbali barani
Afrika, baadhi ya nchi hizo ni wenyeji Afrika ya Kusini, Ivory Coast, Morocco,
Msumbiji, Cameroon, Rwanda, Angola, DRC, Nigeria, Ghana na
Tanzania.
“Ni maonyesho ya pekee na
yenye heshima yake barani Afrika na hata duniani kwa ujumla kwani wabunifu
walioalikwa ni wazoefu na bora katika fani ya Mitindo barani Afrika. Hivyo
mwaliko wangu si tu utaweza kutangaza kazi ni nazofanya bali pia utasaidia
kutangaza nchi yetu ya Tanzania kupitia maonyesho haya” Alisema, Mustafa
Hassanali.
“Watakapotaja jina langu
pale katika maonyesho, hawatasema tu huyu ni Mustafa Hassanali, bali watasema
huyu ni Mustafa Hassanali kutoka Tanzania, hivyo itakuwa ni mchango mkubwa kwa
nchi yetu kuweza kuonyesha fursa zilizopo kupitia Ubunifu wa Mitindo.
Nimejiandaa vizuri katika haya maonyesho, nataka kuonyesha nini Tanzania tunacho
katika tasnia ya ubunifu kwa ulimwengu mzima ni imani yangu kufanya vizuri”
Aliongeza Hassanali.
AFI inaandaa mashindano
haya ili kuweza kutangaza kazi za wabunifu wa mavazi kutoka barani Afrika katika
soko la dunia kwani Afrika ina wabunifu wazuri na imara hivyo kujitokeza kwao
katika maonyesho haya kutafungua milango zaidi katika soko la kimataifa na
kuongeza fursa nyingi zitakazoinua uchumi wa bara hili kupitia sanaa ya ubunifu
wa mitindo.
Licha ya kushiriki katika
maonyesha haya, Mustafa Hassanali pia anawaomba Watanzania wote kwa ujumla
kuweza kumpigia kura ya kuwa mwanamitindo bora barani Afrika kupitia tovuti yawww.awardnomination.afi.za.com na
kuweza kuiletea sifa tasnia ya mitindo nchini Tanzania.
Huu ni mwaka wa tisa kwa
Mustafa Hassanali kupata mwaliko wa kuonyesha ubunifu wake katika maonyesho
haya. Ameshashiriki katika maonyesho zaidi ya nchi 16 katika miji 25 tofauti
duniani, amekuwepo katika kilinge cha sanaa ya mitindo kwa muda mrefu hapa
nchini, amechangia kwa kiasi kikubwa mabadiliko na maendeleo ya kazi za ubunifu
wa mavazi hapa Tanzania.


Post a Comment