Mhe. Naibu Waziri ameitaka TEMESA
kuangalia vyanzo vingine vya mapato, ikiwa ni pamoja na kuongea na
Taasisi za Fedha ambazo zinamasharti nafuu ya mikopo ili kuongeza mtaji
wake. Aidha, Naibu Waziri amehaidi kulivalia njuga suala la madeni
ambalo taasisi hiyo imekuwa ikizidai Wizara na Idara mbali mbali za
Serikali, hata ikibidi kuongea na Hazina ili fedha za madeni hayo
zikatwe moja kwa moja kutoka Hazina. Vile vile ameitaka TEMESA kujenga
hoja kwa vivuko ambavyo vinaendeshwa kwa hasara ili Serikali iangalie
gani inaweza kuwasidia hata kupitia kwenye Halmashauri husika.
Aliongelea usafiri wa boti kati
ya Dar na Bagamoyo Mhe. Naibu Waziri ameiomba TEMESA kuharakisha
mchakato huo ili huduma hiyo iweze kuanza mara moja.
Awali akimkaribisha Mhe. Naibu
Waziri kuongea na Wafanyakazi, Mtendaji MKuu wa Temesa Eng. Marcelin
Magesa alizitaja changamoto mbali mbali zinazokabili wakala huo ikiwa
ni pamoja na kutolipwa madai yao kwa wakati, kwa huduma zinazotolewa na
TEMESA. Upungufu wa watumishi kutokana na wengi kustaafu na wengine
kufariki na kuwa mchakato wa Serikali unachukua muda mrefu. Changamoto
nyingine ni kuwepo kwa mapato kidogo kwenye baadhi ya vivuko kiasi cha
kutokidhi gharama za uendeshaji. Mtendaji Mkuu huyo wa TEMESA ameiomba
Serikali iangalie uwezekano wa kuipatia taasisi hiyo mtaji ili imudu
kukabiliana na changamoto hizo pamoja na ubovu wa karakana na uhaba wa
vitendea kazi katika karakana zote nchini zinazo simamiwa na TEMESA
Wakati huo huo akizungumzia suala
la Dar – Bagamoyo ferry Mtendaji Mkuu alisema tayari Wizara ya Ardhi
imeshatoa Ramani kwa ajili ya maeneo ya maegesho na tenda kwa ajili ya
kumpata Mhandisi Mshauri zimefunguliwa jana Jumatano tayari kwa kuanza
kazi hiyo.
Taarifa Hii imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma
Wizara ya Ujenzi


Post a Comment