***********************
KAMATI ya Bunge ya Hesabu
za Mashirika ya Umma (POAC) imeliagiza Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kufuata
Sheria ya Manunuzi ya Umma (PPRA) katika utendaji wake wa
kazi.
Kauli hiyo ilitolewa leo
na Mwenyekiti wa POAC,Kabwe Zitto wakati kamati hiyo ilipokutana na baadhi ya
viongozi kuhusu kuzungumzia utendaji wa shirika hilo kwenye ukumbi wa ofisi
ndogo ya Bunge jijini Dares Salaam.
Maagizo hayo yalitolewa
na kamati hiyo kufuatia shirika hilo katika mwaka wa fedha 2010/2011 lilipanga
kutumia sh.bilioni 31 lakini limetumia sh. bilioni sh. bilioni 25 nje ya
taratibu za PPRA.
Akijibu hoja hiyo,
Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Nehemia Msechu alisema suala hilo limetokana
nakuwepo kwa miradi ya dharura iliyoangalia masuala ya kibiashara. Hata hivyo
alisema eneo hilo ni moja ya changamoto wanayokabiliana nayo, hivyo wameshaanza
kuifanyia kazi kushirikiana na PPRA.
Kamati hiyo pia imelitaka
shirika hilo, kuwakilisha matumizi ya fedha ya mwaka huu unaoishia Juni, 2012
kwa kuonesha mchanganuo sahihi kabla kikao kijacho na kubadilisha mfumo wa
utaratibu wa malipo ya fedha taslimu,badala yake watumie benki ili kulinda
mapato ya shirika.
Aidha Mwenyekiti wa kamati
hiyo alilipongeza shirika hilo kwa kwa kujiendesha kifaida kutoka sh. bilioni
tatu hadi kufikia sh.bilioni sita na thamani ya mali za shirika hilo kwa sasa
imefikia sh. trilioni 1.75.
Zitto aliongeza kuwa
shirika hilo linatakiwa kuendelea mchakato wa kujiendesha kama kampuni ili
liweze kupata mtaji wa kutosha.
Kamati hiyo ilitaka shirika
hilo, kuzingatia mpango wa kujenga nyumba zenye gharama nafuu kwa watu wenye
kipato cha chini hususan maeneo ya vijijini.
Post a Comment