Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akisaini Kitabu
cha Wageni kilichopo ubalozini hapo.
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akizungumza na
Watanzania waishio nchini Uingereza (hawapo pichani) katika mkutano uliofanyika
hivi karibuni kwenye Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini
humo.
Waziri
Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza,Mh.
Peter Kallaghe wakati akiwasili kwenye ofisi za Ubalozi nchini Uingereza
alipofika kukutana na kuzungumza na Watanzania waishio nchini humo.Katikati ni
Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda.
Siku ya
jumanne tarehe 16.10.12 Mh Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Kayanza Peter Pinda alipata fursa ya pekee ya
kukutana na baadhi ya watanzania waishio nchini Uingereza katika ofisi za
Ubalozi wetu zilizopo hapa jijini London ili kuongea, kufahamiana nao na kuwapa
taarifa kamili kuhusu hali ya nchi Kiuchumi, Kisiasa, Kiusalama, Kimaendeleo na
changamoto mbalimbali zinazozikabili taifa
letu.
Mh Waziri Mkuu alieambatana na mkewe mama Tunu Pinda
walipokelewa rasmi na Mh Balozi wetu Peter Kallaghe, wafanyakazi pamoja na
maofisa kutoka ngazi mbalimbali katika Ubalozi wetu. Kabla ya kuanza hotuba yake
Mh Balozi alichukua fursa hii kuwakaribisha na kuwashukuru watanzania wote ambao
waliojitokeza kuja kumsikiliza na kumsalimia Mh Waziri
Mkuu.
Akihutubia watanzania zaidi ya mia tatu Mh Waziri
alianza kwa kuongelea hali halisi ya uchumi nyumbani ambayo inaendelea kukua
vizuri taratibu siku hadi siku tokea Mh Raisi Jakaya Mrisho Kikwete aingie
madarakani mnamo mwaka 2005. Kutokana na twakwimu za hivi kutoka idara ya uchumi
zinaonyesha kukua kwa GDP kutoka asilimia 6.9% mpaka 7% kwa sasa ambayo
imesababishwa na upanukaji kiuchumi. Vile vile pato la wastani kwa mtanzania wa
kawaida linazidi nalo kuongezeka taratibu japokua sio kwa kasi kubwa kama
ambavyo ingetakiwa. Kwa sasa Mtanzania wa hali ya chini anaishi chini ya dolla
moja ($1.00) kwa siku.
Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 imedhamiria kuwa
Tanzania iweze kunyanyuka na kuingia katika ngazi ya Kati au Middle Income
Country ifikapo mnamo mwaka 2025.
Mwaka 2011-2012 changamoto kubwa ambayo imekua
ikikabili Taifa letu ni mfumuko wa bei za vyakula hususani mahindi, Mchele,
sukari ambayo imetokana na uuzwaji wa vyakula kwa nchi jirani kama Kenya,
Somali, na Sudani ya kusini kwa bei ya ghali na kufanya gharama kuongezeka
nchini. Pia kumekuwepo kwa njaa nchini
katika wilaya ya kaskazini, kanda ya ziwa na Shinyanga ingawaje hatua madhubuti
zimeshachukuliwa ili kuhakikisha tunajitosheleza kwa chakula na zaidi ya hapo kuwekuwepo na mikakati mizuri
itaiwezesha Tanzania kuwa ''Bread Basket kwa East Africa'' kwa kulisha sehemu
nchi zingine katika jumuiya ya Afrika
Mashariki
Tatizo la umeme ambalo bado limekua sugu
linasababishwa na kupanda kwa gharama za mafuta ya
uendeshwaji.
Mapato ya ndani yanazidi nayo kuongezeka mfano TRA
mwaka 2000 walikua wanakusanya bilion 64 kwa mwezi wakati sasa hivi makusanyo ni
kiasi cha sh bilion 650 kwa mwezi japokua mahitaji ya nchi ni makubwa mno kuliko
mapato yanayokusanywa. Pia mauzo ya nje nayo yanazidi ya
zamani.
Uwekezaji wa ndani ya nchi ni Doller 900 ($900
ml)
Ili kukabiliana na hizo Changamoto zinazozidi kukua
siku hadi siku Tanzania imejipanga vizuri ili kuimarisha uchumi na maendelo kwa
ujumla. Mh Raisi Kikwete amerejesha timu ya mipango inayosimamiwa Dr Mipango
ambaye ndio mtendaji mkuu ili kuhakisha mipango yote inayopendekezwa ifanyike
kama ilivyopangwa.
Tanzania imeweka mipango ya muda mrefu ambayo ni miaka
kumi na tano (15) ijayo. Miaka hiyo nayo imegawanywa katika kipindi cha miaka
mitano mitano ili kutekeleza azma yake kwa ufanisi zaidi. Mh Waziri Mkuu
aliendelea kufafanua kuwa Agenda kuu ya miaka hii mitano ya kwanza Tanzania
vipaumbele vimewekwa katika sekta zifuatazo:
a) Ujenzi na upanuzi wa Miundo Mbinu kama Barabara,
Reli, Bandari, Viwanja vya ndege, Nishati na mkondo wa
Taifa
b) Kilimo- Kuongeza zana za kilimo bora kama matrekta,
Mbolea, mbegu bora na kuwawezesha wakulima wadogo wadogo kutumia teknolojia mpya
ya kilimo pamoja na kilimo cha umwagiliaji.
c) Kuwekeza na kujenga Viwanda ( Processin
Industry)
d) Maji safi na
Taka
e) Rasilimali watu
Serikali ya Tanzania imedhamiria kuongeza megawati wa
umeme toka zilizopo sasa hivi ambazo ni megawati 600 mpaka megawati 2780 ndani
ya miaka ijayo ili kuweza kukomesha tatizo la mgao wa umeme ambalo lina gharimu
taifa letu fedha nyingi na kurudisha maendeleo nyuma. Bandari ya Dar inapanuliwa
pia ujenzi wa bandari mpya ya Bagamoyo umeshakamilika pesa na mkandarasi
vimeshapatikani imebakia kuanza kazi.
Tanzania kuwekua na wimbi kubwa la uwekezaji ambapo
nchi nyingi za magharibi zinakimbilia kuja kuwekeza nchini kwetu hasa baada ya
kugundulika kwa gesi, makaa ya mawe, dhahabu na Uranium
nyingi.
Katika kuhitimisha hotuba yake Mh Waziri Mkuu
aliongelea hali ya kisiasa nyumbani na usalama. Kwa ujumla Tanzania bado ni
kisiwa cha amani na utulivu kulinganisha na sehemu zingine ingawaje alizungumzia
matukio mbalimbali ya hivi karibuni ya vurugu kama ya kuchoma makanisa mbagala,
na visiwani Zanzibar, mauaji ya raia wakati wa maandamo Morogoro, Arusha na ya
mwandishi wa habari David Mwangosi alieuwawa na polisi pamoja na mauaji ya
kutisha ya RPC Barlow Mwanza. Mh Waziri Pinda aliwaomba na kuwasihi watanzania
wote kuendelea kufuata sheria pia kuwa watulivu manake mambo yote yamefikishwa
mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake. Pia aliwaushuri watanzania wasiogope
kurudi nyumbani mara wamalizapo masomo au kuwekeza zaidi nyumbani ili kuweza
kujenga taifa letu
Mwishoni kulikuwa na kipindi kirefu cha maswali na
majibu ambapo watanzania mbalimbali walipata fursa ya kumwuliza Mh Waziri Mkuu
maswali na kutoa maoni au mapendekezo yao kuhusu kero na
madukuduku.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WABARIKI
WATANZANIA
Asanteni
Post a Comment