Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa wa benki ya NMB, Kees Verbeek akifafanua jambo wakati wa mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jan kuhusu benki hiyo kudhamini mashindano ya gofu ya ‘NMB Nyerere Masters’ yatakayoanza Oktoba 13-14 katika Viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam. Kulia ni Ofisa Utawala wa TGU, Sophia Nyanjera na kiongozi wa Chama cha mchezo wa gofu Tanzania (TGU), Meja Samuel Hagu
…………………………………………………………
NMB imekua mbele katika kuchangia soka Tanzania, kwa miaka mitano mfululizo NMB imedhamini maendeleo ya soka nchini.Udhamini huo uligawanyika katika kuendelza soka ya vijana na timu ya Taifa. Kwa kwendeleza soka, Leo hii NMB imetangaza udhamini wa shilingi milioni 15 kwa chama cha mchezo wa gofu Tanzania kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya ‘NMB Nyerere Masters’
Mashindano ya Gofu ya NMB Nyerere Masters yamekuwa yakichezwa kwa takribani miaka 12 kwa kumuenzi Baba wa Taifa Mwl.Julius Nyerere. Hili ni shindano lenye hadhi katika nchi yetu.
Mashindano haya yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Oktoba 13-14 katika Viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam,yamewavutia washiriki mia moja kutoka sehemu mbalimbali nchini kama: Frank Roman na Abbas Adam kutoka klabu ya Moshi, Jimmy Mollel na Nuru Mollel kutoka klabu ya Gymkhana Arusha. wengine ni Sherida Chilipachi kutoka Morogoro na Fatma Makame kutoka Dar es Salaam. Washiriki hao watashindania zawadi mbali mbali.
NMB ndio benki pekee ya kwanza yenye matawi zaidi ya 140 na ATM zaidi ya 450 nchini, imekuwa kinara katika ubunifu Tanzania kwa kuanzisha akaunti mpya nyingi na ndiyo benki ya kipekee iliyopo takribani wilayani kwa asilimia 95 ya wilaya nchini.
Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa wa benki ya NMB, Kees Verbeek akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 15 kwa kiongozi wa Chama cha mchezo wa gofu Tanzania (TGU), meja Samuel Hagu kwa ajili ya mashindano ya ‘NMB Nyerere Masters’
Afisa Mkuu wa Wateja Wakubwa wa benki ya NMB, Kees Verbeek akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh milionmi 15 kwa kiongozi wa Chama cha mchezo wa gofu Tanzania (TGU), Meja Samuel Hagu kwa ajili ya mashindano ya ‘NMB Nyerere Masters’ Kushoto ni Meneja Mawasiliano waNMB, Josephine Kulwa na Ofisa Utawala wa TGU, Sophia Nyanjera.
Post a Comment