Katika mahojiano
exclusive na gazeti la Vanguard la nchini Nigeria, Peter na Paul
wamesema
“Basi, ni
mbaya sana kusikia kuwa watu wanatushutumu kwa kuhusika na kifo cha mama yetu.
Hatumlamu mtu yeyote. Watu wako huru kusema chochote wanachotaka kusema.
Tunashangaa kama kuna kitu chochote kitakachotufanya tuchukue maisha ya mama
yetu mpendwa.
Maisha yake hayawezi
kupimwa kwa fedha na umaarufu. Hivyo jibu letu kwa swali hili ni kwamba
hatuhusiki na kifo cha mama yetu. Tunakilaumu tu kifo kilichomchukua mbali nasi
ambacho kama si chenyewe watu wasingekuwa wanatunyooshea vidole. Alifariki baada
ya ugonjwa wa muda mfupi.”
Post a Comment