Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RAIS DKT. SHEIN AZINDUA UTANDAZAJI WA WAYA MPYA WA UMEME ZANZIBAR


 
Meli kubwa yenye jina la FUKADA SALVAGE ikifanyakazi ya kuutandaza Waya Mpya wa Umeme utakaotokea Tanzania Bara mpaka Zanzibar,hafla ya Uzinduzi wa utandikaji wa Waya huo imefanyika huko Fumba Wilaya ya Magharibi Unguja.PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANIZBAR

                                       ***************************
Na Ali Issa Maelzo Zanzibar   

 Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Zanzibar DR Ali Muhamed Sheni amesema kukamilika kwa  jitihada za kulaza waya mpya wa  umeme kutoka Fumba hadi Rasi Kilomoni Dar es salaam wazanzibari wataondokana na tatizo la umeme wa mgao linalo endelea hivi sasa.

 Hayo ameyasema leo huko Fumba wakati wa uzinduzi wa laini mpya ya umeme unao tarajiwa kumalizika Disemba mwaka huu na kutoa huduma kwa wananchi wa Zanzibar ambao kwa muda mrefu wanatumia  nishati hiyo ya umeme wa mgao .

 Amesema hali hiyo itamalizika muda mfupi tu kwani umeme unaolazwa waya wake una megawati 100 ambao utatosheleza mahitaji ya wazanzibari bila ya wasiwasi wowote.

 Amesema hali hiyo ni ya kufurahisha kwa wazanzibari kwani itaifanya Zanzibar kuendeleza shughuli zake za kimaendeleo na kuinua uchumi zaidi bila upungufu wa huduma hiyo .

 “Waya uliopo una megawati 45 ambayo ni ndogo kwa matumizi ya wananchi lakini kukamilika kwa waya huu mpya kutatosheleza mahitaji  ya watu na katika mazingira ya kawaida  si rahisi umeme kukosekana ”ali sema Rais DR. Shein .

 DR. Shein aliwasihi wananchi kukubali kupokea na kutunza huduma hiyo kwa mashirikiano kuazia ngazi ya shehia Wilaya Mikoa na  Taifa kwa kuepuka kujenga ,kuchota mchanga na kadhalika karibĂș na nguzo za umeme .

 Aidha Rais  huyo alishukuru serikali ya Marekani kupitia shirika lake la changa moto za milenia (MCA Compact) ,seriaki ya Japan kampuni ya VISCAS kwa matengenezo ya waya huo na kuulaza baharini.   

 Waya huo  wenye urefu wa kilomita 36.5 una njia za mawasiliano 24 kupitia mshipi teknohama (Febre Optic),una uwezo wa kuishi miaka 40.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top