Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RAIS WA ZANZIBAR DK ALI SHEIN AWAAPISHA MJUMBE (MBM), NAIBU MAWAZIRI NA NAIBU KATIBU WAKUU WA WIZARA MBALI MBALI IKULU ZANZIBAR LEO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akimuapisha Mhe,Saidi Mohamed Said,kuwa Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi, wakaati wa hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar, leo mchana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akimuapisha CDR Julius Nalimy Maziku,kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Idara Maalum za SMZ katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akimuapisha Bw Juma Ameir Hafidh,kuwa Naibu Katribu Mkuu Ofisi ya Rais (Fedha Uchumi na Mipango ya Maendeleo), katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akimuapisha Bw Mustafa Aboud Jumbe,kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Makaazi,Maji na Nishati, katika haflailiyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar, leo mchana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akimuapisha Bw Tahir M. Abdulla,kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano,wakati wa hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar, leo mchana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akimuapisha Mhe.Shawana Bukheti Hassan, kuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi wakati wa hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akimuapisha Mhe, Mtumwa Kheir Mbarak,kuwa Naibu Waziri Kilimo na Maliasili, wakati hafla iliyofanyika Ikulu MjiniZanzibar leo.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu-Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohd Shein akiwa katika Picha ya Pamoja na Mawaziri na Manaibu Makatibu wakuu aliowaapisha leo Ikulu Mjini Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein leo amewaapisha Mawaziri na Manaibu Makatibu Wakuu aliowateua hivi karibuni
Walioapishwa ni Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri asiyekuwa na Waizara maalum Shawana Bukheti Hassan,Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mohamed Said na Naibu Waziri wa Kilimo na Mali Asili Mtumwa Kheir Mbaraka
Wengine walioapishwa na Dkt.Shein ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Taahir Mohamed Khamis,Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,Makazi,Maji na Nishati Mustafa Aboud Jumbe.
Pia aliwaapisha Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais Fedha,Uchumi na Mipango ya Maendeleo Juma Ameir na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi anayeshighulikia Idara Maalum za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar CDR Julius Nalimy Maziku.
Miongoni mwa viongozi ambao walitarajiwa kuapishwa leo na hawakuwepo ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,Makazi,Maji na Nishati Ali Khalil Mirza na Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Dkt Juma Malik Akili
Shuguli hiyo ambayo ilifanyika Ikulu mjini Zanzibar ilihudhuriwa na Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Shariff Hamad,Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd,Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho, Mawaziri mbalimbali,Washauri wa Rais, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Maalim Abdalla Mwinyi Khamis,Kadhi Mkuu wa Zanzibar Khamis Haji,Maofisa wa ngazi mbalimbali za Serikali, pamoja na baadhi ya Wakuu wa Vikosi vya SMZ.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top