S.H. KOVA – DCP KAMANDA WA POLISI
KANDA MAALUMU YA POLISI DAR ES SALAAM AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KATIKA
KITUO KIKUU CHA POLISI KATI LEO
Jeshi
la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limemtia mbaroni Katibu wa Jumuiya
tajwa hapo juu maarufu kama PONDA ISSA PONDA kwa makosa mbali mbali ya
kuchochea vurugu na uvunjaji wa amani jijini Dar es
Salaam.
Aidha
hivi karibuni Sheikh Ponda Issa Ponda aliongoza kundi la wafuasi wake na kuvamia
kiwanja No. 311/3/4 BLOCK “T” eneo la Chang’ombe katika Manispaa ya Temeke mali
ya Kampuni ya AGRITANZA ambayo ipo chini ya Kurugenzi ya Kampuni hiyo. Mnamo
tarehe 12/10/2012 Ponda Issa Ponda aliwaongoza wafuasi wake walioteka eneo hilo
wakidai kwamba wanakomboa.
Mali
za Waislamu, zilizouzwa na BAKWATA, uchunguzi wa awali umeonyesha kwamba kiwanja
hicho kina hati miliki No. 93773 uliotolewa na Wizara ya Ardhi pamoja na
mikataba mbali mbali ya kuuziana au kubadilishana kati ya BAKWATA na Kampuni
tajwa hapo juu. Pia uongozi wa BAKWATA umeletamashahidi kuthibitisha uhalali wa
kiwanja hicho kumilikiwa na Kampuni tajwa. Hivyo watu wote waliovamia eneo hilo
wakiongozwa na Sheikh Ponda wanakabiliwa na shtaka la kuingia kwa jinai pamoja
na uharibifu wa mali katika eneo hilo. Sambamba na kukamatwa kwa Sheikh Ponda
tarehe 16/10/2012 saa 4.00 usiku karibu na eneo la maficho yake ambapo aliletwa
na pikipiki.
WATU
38 WAMEKAMATWA KWA KOSA LA KUINGIA KWA
JINAI
NA UHARIBIFU
Wakati
huo huo sambamba na kukamatwa kwa Sheikh Ponda Issa Ponda Polisi walifanya
operesheni maalumu ya kuwaondoa wavamizi katika kiwanja tajwa hapo juu
kinachomilikiwa na Kampuni AGRITANZA. Watu wapatao 38 walikutwa katika eneo la
kiwanja hicho ambacho kati ya hao (7) ni wanawake na 31 ni
wanaume.
Operesheni
hiyo ilifanyika tarehe 17/10/2012 usiku wa manane kuanzia saa tisa hadi saa kumi
na nusu usiku kwa muda wa dakika 90. Katika eneo hilo vilikutwa vielelzo mbali
mbali vikiwemo visu na mapanga na pia nyenzo mbali mbali za ujenzi, pamoja na
vifaa vya ujenzi, vielelezo hivyo vimehifadhiwa katika kituo cha Polisi tayari
kwa ajili ya ushahidi mahakamani.
SHEIKH
PONDA KUSABABISHA VURUGU NA VITISHO
Katika
siku za hivi karibuni Sheikh Ponda Issa Ponda amekuwa akiwaongoza wafuasi wake
chini ya Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania kwa kufanya maandamano kinyume
cha Taratibu na kuhamasisha umwagaji damu jijini Dar es Salaam na nchini
Tanzania kwa ujumla.
Kwa
ujumla Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania inayoongozwa na Sheikh Ponda
haijasajiliwa kisheria lakini wanatihumiwa kwa uchochezi wa hali ya juu ambapo
licha ya kufanya maadamano kinyume na sheria pia siku ya tarehe 12/10/2012
walisababisha kuvunja kwa makanisa zaidi ya manane, uharibifu wa magari na wizi
au upotevu wa vifaa katika makanisa, yote hayo yameongozwa na Sheikh Ponda na
madhara yake ni makubwa.
Sheikh
Ponda amekuwa mstari wa mbele kupambana na vyombo vya dola pamoja na kuingilia
uhuru wa Mahakama kwa kudai watuhumuwa waliokamatwa kwa uvunjaji wa makanisa na
kufikishwa mahakamani waachiwe mara moja kabla siku saba na kadhalika. Uchunguzi
wa watuhumiwa wote 39 unaendelea na kufikishwa mahakamani mara baada ya
kupitishwa na wakili wa Serikali kuthibitisha mashitaka.
S.H.
KOVA – DCP
KAMANDA
WA POLISI
KANDA
MAALUMU YA POLISI
DAR
ES SALAAM
Post a Comment