Picha na
Maktaba Barabara ya Darajani Visiwani Zanzibar. Askari wa kutuliza ghasia
wameshaanza kurusha mabomu ya machozi kutawanya kundi la uamsho ambao wapo
Barabara ya Darajani wanachoma matairi na kurusha mawe kwa askari. Fujo hizo
zimetokana na kukamatwa kwa kiongozi wa Uamsho Sheikh Farid.
Huyu
ndiye Kiongozi wa Kundi linaloitwa UAMSHO la Zanzibar Sheikh Farid
anayesadikiwa kukamatwa huko Visiwani Zanzibar. Kundi hilo shughuli zake ni za
mihadhara ya Kidini hasa ya Kiislam.
- Kwa mujibu wa Katibu wake, Abdallah Said Ally, amesema alikuwa na dereva wake maeneo ya Michenzani akitokea nyumbani kwake Mbuyuni, ndipo akakutana na gari moja ambalo dereva halifahamu na akashuka mwenyewe kwenye gari lake na kuingia katika hilo gari na kuanzia hapo hadi sasa hajulikani alipo.
- Katibu huyo wa Uamsho na wenzake wamekuwa katika juhudi za kutuliza jazba za wafuasi wao na sasa wanawasiliana na polisi kujua alipo kiongozi wao.Habari zaidi baadae
Post a Comment