Matukio mbalimbali wakati
wamwaliko wa chakula cha jioni kwenye nyumba ya Tanzania ( Tanzania
House)kilichoandaliwa na Mhe. Balozi Salome sijaona baada ya mikutano ya IMF na
WB kumalizika.
Pichani juu ni wajumbe
kutoka Tanzania waliohudhuria mikutano ya IMF na WB Jijini Tokyo- Japan wakiwa
katika mwaliko rasmi wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Mhe. Balozi Salome
Sijaona katika ubalozi wa Tanzania. Kutoka kilia ni Kamishna wa Bajeti Bi.
Monica Mwamunyange, katikati ni Mhasibu Mkuu wa Serikali Bi. Mwanaidi Mtanda na
wakushoto ni Kamishna wa sera Bw. Bedason Shallanda, wakimsikilisa kwa makini
Balozi, hayupo kwenye picha..
Mhe. Balozi Salome sijaona
akiwapokea wajumbe waliokuwa wakihudhuria mikutano ya IMF na WB hapa nyumbani
kwake kwenye ubalozi wa Tanzani ( Tanzania House) kwa chakula cha jioni
alichowaandalia.
Balozi wa Tanzania nchini
Japan Mhe. Salome Sijaona akimkaribisha rasmi Waziri wa Fedha pamoja na ujumbe
kutoka Tanzania kwa chakula cha usiku. kutoka kulia ni Mhe. William Mgimwa
Waziri wa Fedha akifuatiwa na Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe. Omary Yusuph Mzee
akifuatiwa na Bw.Selivicius Likwilile Naibu Katibu Mkuu Wizara na Fedha na
wengineo ni viongozi waliohudhuria hafla hiyo Jijini Tokyo – Japan.
0196-
Wajumbe wa mkutano wa IMF na
WB wakimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini Japan Mhe. Salome Sijaona alipokuwa
anatoa historia fupi ya ubalozi wa Tanzania. 0205
Balozi wa Tanzania nchini
Japan Mhe. Salome Sijaona akimwelezea Waziri wafedha Mhe William Mgimwa mambo
muhimu ambayo yanapaswa kufanyika katika Balozi zetu.
Post a Comment