Mmoja
wa wafuasi wa kikundi cha waislamu wenye imani kali akidhibitiwa na polisi mara
baada ya kukamatwa leo katika kituo kikuu cha polisi Kati wakijaribu kuandamana
ili kushinikiza kiongozi wao Katibu wa Taasisi za Kiislamu Shekh Ponda Issa
Ponda kuachiwa na jeshi la polisi mara baada ya kukamatwa jijini Dar es salaam
kwa kudaiwa kusababisha vurugujijini Dar es salaam.Mwandamanaji mwingine akipelekwa katika kituo kikuu
cha polisi kati jijini Dar es salaam leo mchana mara baada ya kukamatwa
akiandamana
Mmoja
wa wananchi akihojiwa na wananchi ili kutoa maoni yake mara baada ya maandamano
hayo kutawanywa na polisi na baadhi ya waandamanaji kukamatwa leo
mchana
Polisi
wakiwa tayari kwa kudhibiti maandamano hayo katika o kikuu cha Reli karibu na
polisi kati jijini Dar es salaam leo mchana.
Watu wanaosadikiwa kuwa ni waumini wa Dini ya Kiislamu, wamekizingira kituo cha Polisi cha kati (Centre Poice) mchana kuu wakishinika polisi kumwachia huru Katibu wa Jumuiya na Taasisi ya Kiislam, SHEIKH ISSA PONDA, ambaye alikamatwa jana jijini Dar es Salaam.
Watu wanaosadikiwa kuwa ni waumini wa Dini ya Kiislamu, wamekizingira kituo cha Polisi cha kati (Centre Poice) mchana kuu wakishinika polisi kumwachia huru Katibu wa Jumuiya na Taasisi ya Kiislam, SHEIKH ISSA PONDA, ambaye alikamatwa jana jijini Dar es Salaam.
Mida hii askari Polisi, tayari
wametanda katika kila kona za maeneo ya katikati ya Jiji, na kuimarisha ulinzi
katika kituo hicho huku mabomu ya machozi yakirindima eneo hilo la Polisi ili
kuwatawanya waumini hao.
Waumini hao wamegoma kuondoa
eneo hilo huku wakitoa tamkoa la kutoondoka hadi hapo atakapoachiwa kiongozi wao
huyo.
Kiongozi huyo ni miongoni mwa
watu 38, wanaoshikiliwa na jeshi la Polisi kwa kuhusika kwa namna moja ama
nyingine katika uchochezi wa vurugu zilizotokea hivi majuzi huko maeneo ya
Mbagala, jijini Dar es Salaam.
*********************************************
JESHI la Polisi Kanda Maalum
ya Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo, imemtia mbaroni Katibu wa Jumuiya ya na
Taasisi za Kiislam,Sheikh Issa Ponda Issa.
Akizungumza jijini Dar es
Salaam leo, Kamanda wa Polisi kanda maalum,Suleiman Kova, alisema kuwa Ponda
amekamatwa kutokana na kukabiliwa na tuhuma mbalimbali ikiwemo uchochezi dhidi
ya Serikali iliyoko madarakani.
Makosa mengine ni uchochezi wa
udini kati ya waislamu na wakristo na ndani ya waislamu wenyewe,kuchochea vurugu
na uvunjifu wa amani jijini.
Tuhuma nyingine ni kulazimisha
watu kufanya maandamano hasa wanawake na watoto,kumtisha kumuua sheikh Mkuu
Mufti Issa Shaaban bin Simba, kujisifia kuingia Makao Makuu ya Jeshi la Polisi
bila ruhusa na uvamizi wa kiwanja.
Tuhuma nyingine ni kuingilia
uhuru wa Mahakama, umwagaji wa damu, uchomaji wa makanisa zaidi ya nane,
uharibifu wa magari, wizi, upotevu wa vifaa vya makanisa.
“Sheikh ponda amekuwa mstari
wa mbele kupambana na vyombo vya dola na kuingilia uhuru wa Mahakama kwa kudai
watuhumiwa waliokamatwa kwa uvunjaji wa makanisa na kufikishwa Mahakamani
waachiwe mara moja kabla ya siku saba”alisema.
Ponda alikamatwa juzi majira
ya saa 4:30 usiku akiwa kwenye pikipiki kuelekea katika maficho yake maeneo ya
Temeke.
“Juzi usiku sijalala kabisa
kuhakikisha oparesheni ya kumkamata inakwenda salama, Ponda ni mjanja sana ila
Serikali ina mkono mrefu kabla ajaingia katika maficho yake Temeke,alijaribu
kukimbia ili atoroke lakini akakamatwa”alisema.
Kova pia alisema kuwa mnamo
Oktoba 12,mwaka huu Ponda aliwaongoza wafuasi wake na kuvamia kiwanja namba
311/2/4 block T chang’ombe mali ya kampuni ya Agritanza kwa madai ya
kulikomboa.
“Ponda akiwa na wafuasi wake
walivamia kiwanja hicho cha agritanza na kudai kuwa wanakomboa mali za waislamu
zilizouzwa na Bakwata,uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa kiwanja hicho kina hati
miliki namba 93773 iliyotolewa na Wizara ya Ardhi pamoja na mikataba mbalimbali
ya kuuziana”alisema
Aidha Kova alisema kuwa
uongozi wa Bakwata ulipeleka mashahidi kuthibitisha uhalali wa kiwanja hicho na
kusema kuwa watu waliovamia wanakabiliwa na shitaka la kuingia kwa jinai pamoja
na uharibifu wa mali.
“kati ya watu 38 tuliowakamta
wanawake ni saba na wanaume ni 31 na tuliwakuta na silaha mbalimbali kama
visu,mapanga,sururu na vifaa vya kuvunjia na vya ujenzi,jenereta na kujenga
jengo la haraka”alisema Kova.
Aidha Jeshi la Polisi limesema
kuwa limemvumilia Ponda kwa muda mrefu na kuwataka watu wanaoandamana kinyume
cha taratib kuacha.
“Nawasifu sana wakristo ni
wavumilivu,wanabusara kwa tukio la mbagala la kuchoma makanisa la sivyo hali
ingekuwa ya hatari na hata hivyo Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu haijasajiliwa
kisheria”alisema.
Kova amewataka wafuasi wengine
wajisalimishe kwani opareheni inaendelea na watawachukulia hatua za
kisheria.
Pia amewaasa wananchi kutumia
akili zao binafsi na kuacha kufuata mkumbo watashughulikiwa.Jeshi la Polisi
linatarajia kumfikisha Mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
Post a Comment