Lile tamasha kubwa kuliko yote hapa nchini,
maarufu kama Serengeti Fiesta ambalo limekuwa likizunguka mikoa ya Tanzania bara
na kufika takribani mikoa 11 sasa linaelekea katika kilele chake katika viwanja
vya Leaders Club jijini Dar es Salaam siku ya jumamosi wiki hii ambapo msanii wa
hiphop kutoka nchini Marekani Leonard Roberts maarufu kama Rick Ross atatumbuiza
katika tamasha hilo.
Akizungumzia ujio wa msanii mkubwa kama huyo
katika mahijiano maalum jijini Dar es Salaam jana, meneja wa bia ya Serengeti
bw. Allan Chonjo amesema tamasha la Serengeti Fiesta limekuwa likifanya vizuri
sana katika mzunguko wake na kwamba watanzania wamekuwa wakifurahia uwepo wa
tamasha hilo kutokana na mafanikio mbalimbali ambayo wamekuwa wakiyapata kila
ilipofika msimu wa Serengeti Fiesta “mwaka huu tutakuwa na Rick Ross na kwamba
watanzania waendelee kujenga imani na Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia bia
yake ya Serengeti Premium Lager, kwani kila kilele cha msimu wa tamasha hili
ndio mwanzo wa maandalizi ya msimu unaofuata”.
Rick Ross ambaye ni mmoja kati ya wasanii
wanaotamba sana katika miondoko ya kurap (hip hop) nchini marekani, atawasili
hapa nchini siku ya alhamisi tayari kabisa kutumbuiza katika maadhimisho ya
kilele cha tamasha la Serengeti Fiesta siku ya jumamosi mwishoni mwa wiki
hii.
Msimu wa Serengeti fiesta ulianzia katika mikoa
ya Kilimanjaro, Tanga, Musoma, Shinyanga, Mwanza, Tabora, Singida, Dodoma,
Morogoro, Mbeya na Iringa ambapo wakazi wake walipata burudani na ladha ileile
ya bia ya Serengeti kabla ya kufikia mwisho wa msimu wake wiki
hii. Wasanii waliburudisha katika tamasha la Serengeti Fiesta
nyanda za juu kusini ni pamoja na Inspector Haroun, Juma Nature, Roma Mkatoliki,
Linah, Amini, Supa nyota Serengeti fiesta 2012 na wengine.
Maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam na
mikoa ya jirani wanatarijwa kumiminika katika viwanja vya Leaders Club
kushuhudia burudani mbalimbali zitakazotolewa na wasanii wa hapa nchini, kabla
ya kilele cha msimu wa ‘BHAAAS’ kumaliziwa na msanii Rick Ross na kundi lake kwa
kiingilo cha shilingi 20,000/= za kitanzania kwa wale watakaonunua tiketi zao
mapema na elfu 25,000/= kwa wale watakaonunu tiketi
getini.
Katika tamasha la Serengeti Fiesta msimu wa
uliopita uliokuwa ukijulikana kama ‘Haina Majotroo’ Kampuni ya bia ya Serengeti
iliwaleta wasanii maarufu ambapo msanii wa muziki wa raga ‘Shaggy’ alitumbuiza
katika uzinduzi wa msimu huo jijini Mwanza na msanii nyota kutoka nchini
Marekani Ludacris alihitimisha msimu wa kwa kuwaburudisha wakazi wa jiji la Dar
Es Salaam na majirani zake kama kawaida katika viwanja vya Leaders
Club.
Umaarufu wa tamasha Serengeti Fiesta umekuwa
ukitengeneza ajira mbalimbali za muda mfupi na kudumu, na pia nyingine
zikianzishwa kupitia Serengeti Fiesta katika maeneo yote ambayo tamasha hilo
lilipata kupita zikiwemo kuibuliwa kwa wasanii chipukizi na baadaye kujitegemea
kimuziki, kujengeka kwa majina ya wasanii mbalimbali ambao hawakupata kufahamika
zaidi kwa mashabiki wa muziki pamoja na kuibuka kwa wasanii wa filamu kupitia
tamasha hili la Serengeti Fiesta,linalodhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti
kupitia bia ya Serengeti Premium Lager.


Post a Comment