Kibaha, Pwani
Aliyekuwa
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM), Wilaya ya Kibaha Mjini, mkoani
Pwani, Bw. Rugemalira Rutatina, aliibuka mshindi wa nafasi ya ujumbe wa
NEC baada ya kupata kura 547 kati ya 681, zilizopigwa na kuwashinda Bw.
Rashid Bagdela (23) na Fratern Kiwango (11).
Wajumbe watano ambao
walichaguliwa kuwakilisha Mkutano Mkuu Taifa ni Bi. Catherine Katele,
Bw. Joseph Chale, Bw. Jumanne Mangala, Bw. Mohammed Mpaki na Fratern
Kiwango.
Nafasi mbili za ujumbe Mkutano Mkuu CCM Mkoa ni Bi.
Hawa Kadibo na Bw. Said Mkuti. Nafasi ya Halmashauri Kuu Wilaya kupitia
UVCCM, waliochaguliwa bila kupingwa ni Bi. Mwamvua Mwinyi, Bw. Joseph
Chale, Bw. Simba Mohammed na Bi. Sophia Mlao ambapo Bw. David Mramba na
Bw. Yusuph Mbonde, walichaguliwa kupitia wazazi.
Wajumbe wa
Halmashauri Kuu kupitia Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Bi. Fatuma
Silingo, Bi. Gertruda Mtiga, Bi. Hawa Kadibo na Bi. Joyce Shauri ambapo
nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Kibaha Vijijini ilikwenda kwa Bw. Hamis
Kanesa.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani, Bw. Mwinshehe Mlao,
alisema viongozi na wanachama wanapaswa kuacha tabia ya ushabiki na
makundi yasiyo na tija.
Uyui, Tabora
Katika
Wilaya ya Uyui, mkoani Tabora, aliyekuwa Naibu Waziri wa Uchukuzi, Bw.
Athuman Mfutakamba, ameshindwa kufurukuta mbele ya Ofisa Mtendaji Kata.
Bw. Beatus Mlolua.
Bw. Mlolua alishinda ujumbe wa NEC baada ya kupata kura 706 dhidi ya 231 za Bw. Mfutakamba.
Dalili
za kushindwa Bw. Mfutakamba zilianza kujionesha mapema wakati
akijieleza na kuomba kura ambapo swali aliloulizwa na mmoja wa wajumbe
lilimfanya ahamaki.
Muulizwa swali alimtaka Bw. Mfutakamba aeleze
kwanini anawania nafasi ujumbe wa NEC, wakati Rais Jakaya Kikwete,
alimtosa katika nafasi yake ya Unaibu Waziri.
Akijibu swali hilo,
Bw. Mfutakamba alisema, “Aliyeniponza ni waziri wangu (Dkt. Omary
Nundu) Rais Kikwete alinionea, kwani mimi ni mchapakazi hodari”.
Nafasi
ya Mwenyekiti wa CCM wilayani hapa, aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo,
Bw. Abdallah Kazwika, ameangushwa baada ya kupata kura 544, wakati Bw.
Mussa Ntimizi alipata kura 769.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa
wilayani humo ni Bw. Joseph Kidaha, Bi. Anifa Kitwana Kondo, Bw. James
January, Bw. David Malecela na Msafiri Abdurahaman.
Katika Wilaya
Mpya Kaliua, Profesa Juma Kampuya alishinda nafasi ya ujumbe wa NEC
wakati katika Wilaya ya Tabora, Bi. Margareth Sitta, akipita bila
kupigwa.
Mkoani Dodoma
Nafasi ya ujumbe wa NEC Wilaya ya Chamwino, mkoani Dodoma ilichukuliwa na Bw. Malecela Samwel John, kwa kupata kura 727.
Bw. John aliwashinda Kusaja Jeremia (33), Mlugu Nassoro (209), Shamsi Hosea (333) wakati Habel Ngoli aliamua kujitoa.
Akitangaza
matokeo hayo, Katibu wa CCM mkoani hapa, Bw. Albert Mgumba, alisema
katika Wilaya ya Kongwa, Bw. Mussa Abdi alichaguliwa kuwa Mwenyekiti CCM
kwa kura 836 na kuwashinda Mbijima Tagwe (44) na Simango Filemond
(327).
Ujumbe wa NEC Wilaya ya Kongwa, mshindi ni Bw. Godwin
Mkanwa (738), ambaye aliwashinda Bw. Mathias Kanyata (117), na Amon
Anderson (334).
Katika Wilaya ya Chamwino, nafasi ya Mwenyekiti
wa Wilaya alichukuliwa na Ulanga Benjamini (776), aliyewashinda Kusaja
Jeremia (54) na Mtweli Malile (58)
Wilaya ya Mpwapwa Bw. John Chigwile alipata kura 794 na kuwashinda Honorati Pima (285) Bw. Said Mguto (255).
Nafasi
ya NEC Mpwapwa, mbunge wa zamani wa jimbo hilo, Bw. George Lubeleje
alipata kura (911) na kuwashinda Bi. Rehema Halala (155) na Clavery
Peter (279).
Katika Wilaya ya Chemba, kulikuwa na mgombea moja wa
nafasi ya Mwenyekiti wa CCM, Alhaji Issa Mlalo, ambaye alipata kura 867
za ndio na 11 zilimkataa.
NEC Wilaya ya Chemba, Bw. Juma Nkamia
alipata kura 602 na kuwashinda Bw. Saidi Sambara (110) na Bw. Fredrick
Duma (121) ambapo katika Wilaya ya Kondoa, kura zilipigwa mara mbili.
Waandishi wa habari hii ni Peter Ringi, Moses Mabura, Cresensia Kapinga, John Gagarini na Pendo Mtibuche.

Post a Comment