Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

RPC Mwanza, Liberatus Barlow auawa kwa Kupigwa Risasi na Majambazi na IGP Mwema atuma kikosi kazi kuchunguza sakata hilo

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow ameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi usiku wa kuamkia leo katika maeneo ya Kitangiri jijini Mwanza.

Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Said Mwema amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema timu ya Makachero kutoka Dar ikiongozwa na Mkurugenzi wa Upepelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba inakwenda jijini humo kuongeza nguvu ya kiupelelezi na taarifa zaidi zitatolewa baadaye.
R.I.P KAMANDA LIBERATUS BARLOW 


WAKATI HUO HUO 
 


IGP Mwema
Mkuu  wa  jeshi la  polisi (IGP) Said Mwema amethibitisha  kuuwawa kwa kakamnda  wa  Mwanza Liberatus Barlow .

Amesema  kuwa  kamanda  huyo wa polisi ameuwawa na  watu  wanaosadikika kuwa ni majambazi majira ya saa 7.30  na saa 8 usiku   katika maeneo ya Kitangiri jijini Mwanza.

Mwema amesema  kuwa kamanda  Barlow alikuwa akitokea katika  kikao cha harusi akiwa njiani kumrudisha dadake nyumbani kwake ghafla  alikutwa na tukio  hilo la  kupigwa  risasi.



Hata  hivyo alisema  kuwa  kutokana na tukio  hilo jeshi la  polisi  linataraji kuanza uchunguzi  wake kuanzia leo na timu ya askari  kutoka  makao makuu ya polisi  wataondoka mapema leo kwenda  jijini Mwanza  kuungana na askari wa mkoa  huo kwa ajili ya uchunguzi  zaidi na msako wa majambazi hayo .


Mwema amewataka  wananchi  wa Mwanza  kutoa ushirikiano wao kwa  jeshi la polisi ili kufanikisha  zoezi hilo na  kuwataka kutokuwa na hofu  yoyote kutokana na tukio  hilo.
 
 
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top