ya Kamati ya Nobel nchini Norway kuridhika kwamba Umoja huo umekuwa
katika mstari wa mbele kupigania na kueneza demokrasia Ulaya na duniani kwa
jumla.
Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Nobel, Thorbjorn Jagland amesema cha
msingi kilichowafikisha katika uamuzi wa pamoja wa kutoa tuzo hiyo kwa
Umoja wa Ulaya ni juhudi za Umoja huo za kuleta amani na maridhiano
pamoja na demokrasia katika Umoja huo baada ya vita vya pili vya dunia
.
Tuzo hiyo inaonekana kama hatua ya kuupa nguvu na mori muungano huo
wakati ukiwa katika mapambano ya kuutatua mgogoro wake wa madeni.
Kamati hiyo imezipongeza nchi wanachama 27 kwa kuujenga upya umoja wao
baada ya Vita vya Pili vya Dunia pamoja na kazi iliyoifanya katika kueneza
utulivu katika nchi zilizokuwa za Kikomunisti baada ya kuangushwa ukuta wa
Berlin mwaka 1989.
Tuzo ya Amani ya Nobel inayoambatana na zawadi ya fedha dola milioni
1.2 itakabidhiwa rasmi kwa Umoja huo katika sherehe itakayofanyika mjini
Oslo, Norway, hapo tarehe 10 Disemba.
Bunge la Ulaya laisifu heshima ya NobelBunge la Umoja wa Ulaya.
mtandao wa Twitter, akisema hatua ya kamati ya Nobel kutambua maridhiano
ya baada ya vita vya pili vya dunia barani Ulaya ni jambo la kutia moyo.
Amesema Umoja wa Ulaya unahusu Maridhiano, Umoja wa Ulaya ni mradi wa
Amesema Umoja wa Ulaya unahusu Maridhiano, Umoja wa Ulaya ni mradi wa
kipekee uliovitenga vita na kuchukua njia ya amani kwa kuleta mshikamano kupambana na chuki.
Umoja huo uliasisiwa mwaka 1957 kupitia mkataba wa Roma ukianzia na
Umoja huo uliasisiwa mwaka 1957 kupitia mkataba wa Roma ukianzia na
wanachama sita waliokuwa na lengo la kutafuta ushirikiano wa kiuchumi na
kufikia sasa ni nchi 27 zinazounda Umoja huo zikiwemo nchi za Ulaya Mashariki zilizojiunga baada ya Vita Baridi.
Hata hivyo, Umoja wa Ulaya umekumbwa na mgogoro huku kukiweko na
Hata hivyo, Umoja wa Ulaya umekumbwa na mgogoro huku kukiweko na
hali ngumu kwenye eneo lake la Sarafu ya Euro inayotumiwa na nchi 17 za
Umoja huo.
Kutoka na hali hiyo tuzo ya amani ya Nobel imekuja kwa mshangao kwa wengi
Kutoka na hali hiyo tuzo ya amani ya Nobel imekuja kwa mshangao kwa wengi
hasa kutokana na mvutano huo wa sarafu ya Euro. Wengi wa Wanorway
wanaupinga Umoja wa Ulaya kwa kuuona kama ni kitisho kwa uhuru wa nchi zinazouunda.
Itakumbukwa kwamba Norway kitovu cha tuzo ya Nobel, imepiga kura mara
Itakumbukwa kwamba Norway kitovu cha tuzo ya Nobel, imepiga kura mara
mbili za kukataa kujiunga na Umoja huo mwaka 1972 na mwaka 1994.
Post a Comment