Katibu wa Jumuiya na
Taasisi za Kiislam,Sheikh Issa Ponda, na watu wengine 50 wakiwa katika Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kujibu mashtaka
mbalimbali
Karandiga lililowabeba
Sheikh Issa Ponda na wenzake
Wanahabari wakiwa
kazini
Wanahabari wakirekodi
kuwasili kwa Sheik Issa Ponda Mahakamani Kisutu leo
Mmoja wa washtakiwa
akitelemshwa kutoka kwenye karandinga
Picha Kwa Hisani ya Michuzi Blog
**************************Katibu wa baraza la Waislam Tanzania Shekhe Issa Ponda amepandishwa kizimbani leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam na kusomewa mashitaka matano.
Alifikishwa mahakamani hapo na kupoandishwa kizimbani na watu
wengine 49 akiwemo bibi wa miaka 100 kwa msafara wa magari ya polisi na ving’ora likiwemo gari la maji ya machozi kwa kasi ya ajabu na kushushwa haraka. Hata hivyo baada ya kukana mashitaka yao walirudishwa rumande baada ya kukosa dhamana.
Wote kwa pamoja walidaiwa kula njama, na katika maelezo ya kosa walidaiwa Oktoba 12, mwaka huu katika eneo la Chang’ombe Markasi katika Wilaya ya Temeke jjijni Dar es Salaam walikula njama ya kutenda kosa.
Shitaka jingine wanadaiwa wote kwa pamoja kuingia kwa nguvu kutaka kufanya makosa, huko huko Chang’ombe kwa jinai na bila sababu za msingi walivamia Ardhi katika kiwanja kinachomilikiwa na kampuni ya Agritanza kwa nia ya kujimilikisha isivyo halali
Shitaka la tatu walidaiwa kujimilikisha kwa nguvu, maelezo ya kosa walidaiwa wote kwa pamoja walivamia kiwanja hicho pasipo kuwa na uhalali na katika hali ya uvunjifu wa amani, walijimilikisha mali hiyo ambayo ni mali halali ya kampuni ya Agritanza
Aidha katika shitaka la nne ambalo ni la wizi kati ya Oktoba 12 na 16 mwaka huu, washitakiwa waliiba vifaa vya ujenzi walivyovikuta katika kiwanja hicho vyenye thamani ya shilingi 59,650,000 ambavyo ni kokoto, nondo na saruji mali ya kampuni ya Agritanza.
Washtakiwa wote walikana mashtaka hata hivyo walirudi rumande kwa sababu hakimu aliyepangiwa kusikiliza kesi hiyo hakuwepo na hivyo kusomwa mbele ya hakimu Sanga ambaye alisema hana mamlaka.
Mkurugenzi wa mashitaka nchini (DPP) amewasilisha hati ya kuzuia dhamana ya Shekhe Ponda kwa kile alichotaja kuwa ni kwa usalama wa Ponda na pia kwa maslahi ya Jamhuri. Kesi hiyo itatajwa Novemba mosi mwaka huu na kwamba upelelezi haujaamilika.
Pamoja na jitihada za wakili wao Juma Nasoro kuwaombea dhamana wateja wake lakini jitahada hizo ziligonga mwamba.

Ponda, aliyewasili peke yake, alipelekwa moja kwa moja
katika chumba cha mahakama na kuunganishwa na washitakiwa wenzake. Wote
walisomewa mashitaka hayo mbele ya hakimu Stewart Sanga na wakili wa serikali
Jumanne Kweka.
Wote kwa pamoja walidaiwa kula njama, na katika maelezo ya kosa walidaiwa Oktoba 12, mwaka huu katika eneo la Chang’ombe Markasi katika Wilaya ya Temeke jjijni Dar es Salaam walikula njama ya kutenda kosa.
Shitaka jingine wanadaiwa wote kwa pamoja kuingia kwa nguvu kutaka kufanya makosa, huko huko Chang’ombe kwa jinai na bila sababu za msingi walivamia Ardhi katika kiwanja kinachomilikiwa na kampuni ya Agritanza kwa nia ya kujimilikisha isivyo halali
Shitaka la tatu walidaiwa kujimilikisha kwa nguvu, maelezo ya kosa walidaiwa wote kwa pamoja walivamia kiwanja hicho pasipo kuwa na uhalali na katika hali ya uvunjifu wa amani, walijimilikisha mali hiyo ambayo ni mali halali ya kampuni ya Agritanza
Aidha katika shitaka la nne ambalo ni la wizi kati ya Oktoba 12 na 16 mwaka huu, washitakiwa waliiba vifaa vya ujenzi walivyovikuta katika kiwanja hicho vyenye thamani ya shilingi 59,650,000 ambavyo ni kokoto, nondo na saruji mali ya kampuni ya Agritanza.
Shekhe Ponda peke yake ameshtakiwa kuchochea kwa nia ya
kuhamasisha utendaji kosa katika maeneo tofauti kati ya Oktoba 12 na 16 mwaka
huu, kama katibu wa baraza la Waislam Tanzania, huko Temeke eneo la Chang’ombe,
jijini Dar es salaam.
Washtakiwa wote walikana mashtaka hata hivyo walirudi rumande kwa sababu hakimu aliyepangiwa kusikiliza kesi hiyo hakuwepo na hivyo kusomwa mbele ya hakimu Sanga ambaye alisema hana mamlaka.
Mkurugenzi wa mashitaka nchini (DPP) amewasilisha hati ya kuzuia dhamana ya Shekhe Ponda kwa kile alichotaja kuwa ni kwa usalama wa Ponda na pia kwa maslahi ya Jamhuri. Kesi hiyo itatajwa Novemba mosi mwaka huu na kwamba upelelezi haujaamilika.
Pamoja na jitihada za wakili wao Juma Nasoro kuwaombea dhamana wateja wake lakini jitahada hizo ziligonga mwamba.
Msafara wa zaidi ya magari
kumi uliondoka na washitakiwa hao huku likiwemo gari lile la maji ya machozi
maaskari wa barabarani, askari magereza na fidifosi huku Ponda akiwekwa katika
gari la vioo vya giza kama
alivyoletwa.
Post a Comment