Afisa uhusiano wa shirika la umeme (TANESCO) Bi.Badra Masoud wakati akizungumza na waandishi wa habari
Tanzania itakuwa mwenyeji
wa mkutano(5) wa mawaziri wanaosimamia nchi Nishati ya Umeme kutoka nchi 11
zilizo Mashariki na Kati mwa Afrika wanaounda mtandao wa nishati na umeme
maarufu kama”East Afrika Power Pool (EAPP) unaotarajiwa kuanza rasmi hapo
kesho.
Hayo yamesemwa na Afisa
uhusiano wa shirika la umeme (TANESCO) Bi.Badra Masoud wakati akizungumza na
waandishi wa habari juu ya mkutano huo mkubwa ambao unatarajiwa kufanyika
jijini Arusha.
Bi.Masoud alisema kuwa
Tanzania ni mwanachama wa mtandao wa (EAPP) ulionzishwa miaka 6 iliyopita ikiwa
na lengo la kurahisisha upitakanaji wa nishati ya uhakika ya umeme kwa nchi
wanachama wa EAPP kwa kujenga njia kuu ya kusafirishia umeme unaounganisha nchi
hizi.
Aidha alifafanua kuwa
Tanzania inahitaji kuboresha maisha ya wananchi wake katika Nyanja nyingi kama
vile matibabu,elimu,upatikanaji wa maji safi na salama,uzalishaji,Ongezeka la
viwanda na kurahisisha matumizi ya majumbani.
Alisema kuwa haya yote
yatawezekana tu kama kutakuwa na umeme wa uhakika na wenye gharama nafuu ili
wananchi waweze kumudu gharama hizo bila matatizo yeyote.
Bi.Masoud alisema ili
kupata umeme wa uhakika na gharama nafuu,Mawaziri wa nchi hizi 11 watatoka na
mwongozo wa utekelezaji wa kuunganisha miundombinu ya njia kuu ya kusafirisha
umeme kwenye nchi za Afrika Mashariki na Kati mwa Afrika.
“Kwa sasa tunanunua umeme
bei ghali sana kutoka kwa wazalishaji binafsi (Independent Power Producer-IPP)
ambao wanatuuzia umeme kwa bei ghali sana hivyo TANESCO inaponunua umeme kwa
bei ghali sana na kuiuza kwa bei kawaida inaipelekea kupata hasara na hata
kupandisha bei ili kukidhi gharama za uendeshaji.”alisema
Badra
Hata hivyo alisema kuwa
mkutano huo utatanguliwa na Wakurugenzi wa mashirika yaliyo na dhamana ya
kuzalisha,kusafirisha na kusambaza umeme,wakiwepo wadau wa Mamlaka za Udhibiti
wa Nishati ya Umeme wataanza mkutano wa awali utakaofuatiwa na mkutano wa
Mawaziri siku ya Jumamosi.
Alisema
kuwa nchi wanachama wa EAPP,ni Tanzania
,Kenya,Uganda,Ethiopia,Rwanda,Burundi,Libya,Egypt,Republic
of Sudan,Demokratic Republic of Congo(DRC) na
Djbouti.
Post a Comment