Spika wa Bunge Mhe. Anne
Makinda akisisitiza jambo aliposhiriki Mdahalo maalumu ulioandaliwa na Chama Cha
Mabunge Duniani (IPU), Mjini Quebec, Canada, kuzungumzia Mabunge yenye Mwitikio
wa kuzingatia Maswala ya Jinsia ikiwa ni sehemu ya kuongeza idadi ya wanawake
Bungeni. IPU walimchagua Mhe. Makinda kubadilishana na wabunge wengine uzoefu wa
Tanzania ikizingatiwa kuwa Tanzania ni moja kati ya Nchi chache zenye
kuzingatia uwiano wa Wabunge wanawake Bungeni Kikatiba. Kulia ni Mwenyekiti wa
Sanate katika Bunge Ireland Mhe. Paddy Burke na Katikati ni mwongozaji wa
Mdahalo huo Bi. Jemini Pandya ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa
IPU.
on Wednesday, October 24, 2012
Post a Comment