NDANI YA HANDAKI HILO KUBWA LILIGUNDULIWA KUMEKUTWA NA NYUMBA KUBWA AMBAYO INASADIKIWA ILIJENGWA NA WAJERUMANI AMBAO NDIO WANASADIKIWA KULICHIMBA HANDAKI HILO.
WATU WENGI WAMEJAA KATIKA ENEO HILO WAKILITAZAMA HANDAKI HILO NA WENGINEO WAMEKUWA NA MALENGO YA KUTAKA KUIBA WAKIWA NA IMANI MAHALI POPOTE PALE WALIPOISHI WAJERUMANI WALIACHA MALI NA WANA IMANI HATA HUMO NDANI KUNA MALI TELE.
POLISI WENGI WAMESHAFIKA KUHAKIKISHA WANAIMALISHA HALI YA USALAMA INAYOONEKANA KUTAKA KUTOWEKA MAHALI HAPO.
IKUMBUKWE YA KUWA MKOA WA IRINGA YALIKUWA NI MAKAZI YA WAKOLONI (HAPO ZAMANI) AMBAO WALISHIRIKI KWENYE HARAKATI YA KUPAMBANA NA CHIFU MKWAWA AMBAYE ALIKUBALI YAISHE KWA KUAMUA KUJINYONGA.
Umati wa watu waliofika
katika eneo la kitanzini kuangalia handaki hilo
mkuu wa Wilaya Ya
Iringa mjioni Dkt Leticia Warioba akihojiana na mmiliki wa numba ambayo handaki
hilo limeonekana
Handaki lenyewe
muonekano wa sehemu ya kuingilia
Mkuu wa Wilaya kushoto
aipokea maelekezo kutoka kwa mmoja wa wafanyakazio wa kampuni ya maji
Iringa
Wananchi wakendelea
kutazama kila mmoja akiwaza lake
Handaki la ajabu
limeonekana katika eneo la kata ya kitanzini mtaa wa
sokoni
Katika tukio hilo
lililokuwa gumzo kubwa katika eneo hilo huku kila mmoja akisema
lake
Mtandao huu ulipokutana
na mmiliki wa nyumba hiyo hakuweza kuwa na majibu yakuridhisha huku akisema
yeye hafahamu shimo hilo limetokea wapi.
Handaki hilo ambalo lilionekana jana na wachimbaji wa mitaro wa JR wanaoshuhulika na uwekwaji wa mabomba mapya ya maji safi wanaeleza katika kuchimba ndipo walipokutana na chemba hiyo ikiwa imefunikwa na kudhani kuwa inatumika kama shimo la choo ya nje lakini haikuwa hivyo maana lilikuwa wazi limejengewa na hakuna dalili ya kutumika kama choo.
Akizungumza mmoja wa wananchi aliyeingia katika handaki hilo Abdukareem ameeleza kuwa yeye ni mkazi wa eneo hilo na alipopata taarifa alifika akiwa na mwenzake aliyefahamika kwa jina la Salehe na kukubaliana kuingia ndani ili kufahamu kilichopo.
Ameeleza kutokana na shimo hilo kuwa refu walitafuta ngazi lakini hawakufanikiwa kwani ngazi hiyo ilikuwa pana na kuamua kutafuta fimbo kubwa ya muanzi na kamba na ndipo walipofanikiwa kuingia ndani.
Anazidi kueleza kuwa walipofika ndani walikuta chumba ambacho ni kama futi tatu na kuona vidirisha vidogo kwa mbele huku bado kukiwa kumejengewa kwa zege na kubainisha kuna muendelezo wa chemba nyingine ambapo hawakuweza kuendelea kutokana na kuzibwa.
mkuu wa Wilaya afika
eneo la tukio
Mkuu wa wilaya ya Iringa Dkt Leticia Warioba akafika katika eneo la tukio huku akiwa na wa wafanyakazi wa Kampuni ya JR pamoja na afisa wa usalama ambao waliishia kuangalia njia hiyo pasipo kuingia ndani ya handaki hilo.
nini maoni ya wakazi
waliofika katika eneo hilo?
Wengi wa wakazi waliofika katika eneo hilo hawakusita kueleza hisia zao huku wengine wakieleza labda ni mahandaki yaliyokuwa yakitumiwa na Wajerumani enzi za ukoloni, huku wengine wakieleza labda handaki hilo limekuwa likitumiwa na majambazi kama sehemu za kujificha na kuhifadhia mali walizoiba japo hapakuonekana na mali aina yeyote.










Post a Comment