Manchester
United leo wamesema kwamba mipango ya kupata mbadala wa Sir Alex Ferguson
imeshajadiliwa na mpaka sasa kila kitu kipo tayari lakini mipango hiyo sasa
imefungiwa kwenye makabati ya ofisi za klabu hiyo huko Old
Trafford.
Makamu mwenyekiti wa Klabu hiyo Ed Woodward amesema kwamba listi ya watakaowania nafasi ya Fergie ipo tayari na wanaijua watu wachache sana lakini hakuna tarehe inayojulikana kuwa ndio itakuwa mwisho wa kocha Mscotland pale Theatre of Dreams.
Alisema: "Tayari tuna mtazamo wa namna mchakato mzima wa kumpata mbadala wa SAF utakavyokuwa na ni aina gani ya mwalimu tunataka na vipi tutampata huyo mwalimu.

'Lakini
kila kitu kuhusu jambo hilo kipo kwenye makabati na mipango yote itakaa huko
hata zaidi ya tunavyofikiria."
Majina
kama Jose Mourinho na Pep Guardiola, vilevile David Moyes, mara nyingi yamekuw
yakihusishwa na kazi ya kumrithi Fergie katika klabu yenye mafanikio kuliko zote
pale Uingereza, japokuwa bado haijajulikana lini babu huyo
atastaafu.
Akiongea
mapema mwaka huu wakati akisherehekea miaka yake yake 25 ndani ya klabu hiyo,
babu mwenye miaka 70 alisema: " Sijui ni muda gani nitaweza kuwa hapalakini kama
afya yangiu itaniruhusu sidhani kama miaka mingine mitatu au miwli itakuwa
shida.

Post a Comment