KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE KUKUTANA DAR KUANZIA TAREHE 15 HADI 26 OKTOBA, 2012
1.0 UTANGULIZI
Kwa
kawaida, wiki mbili kabla ya Mkutano wa Bunge, Kamati za Kudumu za
Bunge hukutana ama Dar es Salaam, Dodoma au Zanzibar kwa mujibu wa
Kanuni ya 114(3) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la 2007. Kuanzia
tarehe 15 hadi 26 Oktoba 2012 Kamati hizo zitakutana Jijini Dar es
Salaam kabla ya Mkutano wa Tisa wa Bunge unaotarajiwa kuanza tarehe 30
Oktoba hadi 09 Novemba, 2012. Hata hivyo Kamati ya Nishati na Madini
haitakuwepo kutokana na kuvunjwa wakati wa Mkutano wa Nane wa Bunge la
Kumi.
Aidha
Wabunge wote wanapaswa kuwa wamewasili jijini Dar es Salaam ifikapo
tarehe 14 Oktoba 2012 tayari kwa kuanza vikao siku inayofuata.
2.0 SHUGHULI ZITAKAZOTEKELEZWA
2.1 Shughuli za jumla:
2.1.1 Uchambuzi wa Muswada mmoja wa Sheria
2.1.2 Kushughulikia maazimio manne ya Bunge
2.1.3 Kupokea Taarifa mbalimbali kutoka Wizara na Taasisi za Umma na Binafsi
2.1.4 Ziara fupi Jijini Dar es Salaam
2.1.5 Ziara ndefu nje ya Dar es Salaam
2.2 Kupitia Hesabu zilizokaguliwa 2010/2011
2.2.1 Hesabu za Mashirika ya Umma
2.2.2 Hesabu za Serikali za Mitaa
2.2.3 Hesabu za Serikali Kuu
2.3 Maazimio ya Bunge
Kamati tatu zitakuwa na kazi ya kushughulikia maazimio manne ya Bunge
kuridhia Mikataba mitatu na Itifaki moja. Kamati hizo ni:-
i) Kamati ya Fedha na Uchumi – Azimio moja la Mkataba
ii) Kamati ya Miundombinu – Azimio moja la Mkataba na moja la Itifaki
iii) Kamati ya Huduma za Jamii – Azimio moja la Mkataba
2.4 Taarifa za Utendaji
Kamati
kumi zitapokea na kujadili Taarifa za Utendaji wa Wizara na Taasisi
zilizo chini yake kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa majukumu ya Serikali kupitia Wizara na Taasisi hizo.
3.0 ZIARA
Kamati
tisa zitafanya ziara fupi na ndefu kwa madhumuni ya kufuatilia
utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya Serikali na Taasisi zake.
Imetolewa na: Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na Uhusiano wa Kimataifa,
Ofisi ya Bunge
Dar es Salaam
10 Oktoba 2012
Post a Comment