Balozi wa Ubalozi wa Kudumu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Tuvako Manongi
akizungumza wakati wa mjadala wa wazi ulioandaliwana Baraza Kuu la Usalama la
Umoja wa Mataifa na kufunguliwa na Katibu Mkuu Ban Ki Moon. Mjadala huo ulihusu
uhusiano kati ya Amani na Haki na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (
ICC) miongoni mwa mambo aliyosisitiza Balozi Manongi ni pamoja na kuishauri ICC
kutenda haki bila kuegemea upande wowote na kwamba ijitahidi kujiepusha na
ushawishi wa kisiasa kutoka nchi yoyote ile likiwamo Baraza Kuu la
Usalama.
Wajumbe wa Baraza Kuu la
Usalama la Umoja wa Mataifa katika mkutano wake wa wazi uliokuwa ukijadili
uhusiano kati ya Amani na Haki na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya
Jinai.
Na Mwandishi
Maalum
Mahakama ya Kimataifa ya
Makosa ya Jinai ( ICC) imeshauria kutekeleza majukumu yake bila ya kushawishi wa
kisiasa kutoka nchi yoyote ile likiwamo Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa
Mataifa. Ushauri huo umetolewa na Tanzania kupitia Balozi wake wa Kudumu wa
Tanzania katika Umoja wa Matiafa, Tuvako Manongi, wakati wa mjadala wa wazi
uliohusu uhusiano kati ya Amani na Haki na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya
Jinai ( ICC).
Mjadala huo uliandaliwa na
Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa. Akizunguma katika mjadala huo
uliofunguliwa na katibu Mkuu wa UM, Ban Ki Moon, Balozi Manongi amesema, ili
Mahakama hiyo iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo inapashwa kujiepusha na
ushawishi au mashikinikizo ya kisiasa.
Akafafanua kwamba, kwa
Tanzania kama ilivyo kwa nchi nyingine ambazo zimekwisha kuitambua mahakama
hiyo, inategemea na inaamini kwamba itatekeleza majukumu yake bila ya upendeleo
wa aina yoyote ile.
Akaeleza wazi kwamba nchi
nyingi hasa zile za Afrika zimekuwa zikionyesha wasi wasi wao juu ya mwenendo wa
Mahakama hiyo licha ya ukweli kuwa , nchini nyingi za Afrika siyo tu zimeitambua
lakini masuala mengi yanayoshughulikiwa na makahama hiyo yanaihusu Afrika. “
Uhuru wa kutoadhibiwa lazima uzingatiwe wakati wowote na mahali
popote”.
Anasema Balozi na kuongeza.
“ Usemi kwa kwamba haki ni lazima itendeke, lakini vile vile lazima ionekane. Na
huu ni ukweli kwa chombo chochote cha kisheria kama inavyotakiwa kufanyika pia
katika ICC”.
Akasisitiza. Na kuongeza
kwamba ili haki hiyo itendeke na kuonekana ni lazima basi iwe kwa wote bilaya
kujali au kuzingatia ushawishi wa kisiasa. Na kufafanua zaidi kwamba mataifa
mengi ya Afrika yanaona kama vile uwajibishwaji katika ICC unalenga upande
mmoja. Na hili ni tatizo ambalo linapelekea ICC kutopata ushirikiano wa
kutosha.
Akaeleza kwamba majukumu
ya Baraza Kuu la Usalama la UM na yale ya ICC kwa kiasi fulani yanashabihiana
kutokana na kweli kwamba asilimia kubwa ya majukumu yao yanaihusu Afrika. “
Jukumu la kutafuta amani na haki ni jukumu la msingi kwa Baraza kuu na hali
kadharika kwa ICC. Na mara nyingi imeelezwa kuwa amani haiwezi kuwapo bila
haki.
Na kwa hakika amani na haki
ni kama pande mbili za sarafu zinazotegemeana, kwa sababu upande mmoja hauwezi
kustawi bila ya mwingine” akasisitiza Balozi Manongi Na kuongeza lakini katika
mazingira Fulani Fulani, Jumuia ya Kimataifa na Baraza kuu la Usalama zimejikuta
zikilazimika kujaribu kutafuta uwiano kati ya pande hizi mbili hasa pale upande
mmoja unapoonekana kuuelemea upande mwingine. “ Ndio maana haishangazi kwamba
kitendo cha kutafuta uwiano kati ya haki na amani kumezua hofu
kubwa.
Kutokana na kwamba ni jambo
lisiloingia akilini kwa mahakama kutafuta haki kwa gharama ya mchakato wa
kutafuta amani. Hata kama itamaanisha kutoa unafuu wa muda kwa watuhumiwa
kutochukuliwa hatua” akasema Balozi Na kusisitiza kwamba, mchakato wa kutafuta
amani kwa namna yoyote ile usilinganishwe na uhuru wa
kutoadhibiwa.
Aidha amelitaka Baraza Kuu
kuwa wazi zaidi kwa kutoa maelezo kwa nchi ambazo zimeomba uahilishaji wa
mashtaka na hii itasaidia kuboresha ushirikiano na kuondoa hisia potofu dhidi ya
ICC. Halikadharika Mwakilishi huyo wa Tanzania katika UM, anasema ICC si chombo
pekee chenye jukumu la kutafuta haki kwa waathirika wa vitendo vya
jinai.
Kwakile alichosema hata
nchi moja moja zinawajibu na haki ya kutafutua haki kwa waathirika kwakutumia
taasisi zake za kisheria, kinachotakiwa ni kuzijengea uwezo wa kutekeleza jukumu
hilo hasa kwa nchi zile ambazo zimetoka katika vita au
machafuko.
Kwa upande mwingine,
Tanzania imelitaka Baraza Kuu kuisaidia ICC kwa maana ya raslimali ili iweze
kutekeleza majukumu yake ya msingi na vile vile kuzishawishi nchi kutoa
ushirikiano kwa mahakama hiyo.
Post a Comment