Katika uchaguzi
wenye ushindani mkubwa na diplomasia ya hali ya juu, nchi nyingi
zilikusudia kuingia kwenye Baraza hilo. Tanzania imekuwa moja ya nchi
mbili za Afrika Mashariki, ikiwamo Uganda kushinda nafasi hizo. Nchi
nyingi e za Africa zilizofanikiwa kuingia katika Baraza hilo ni
Burkinafaso, Jamhuri ya Congo Brazaville, Ivory Coast, Misri, Gabon,
Malawi, Morocco, Sudan na South Africa.
Mapema leo
asubuhi, Balozi Hussein A. Bishar wa Kenya alichaguliwa kuwa Mkurugenzi
Mtendaji wa UPU akimshinda mwanamama Serrana Casco kutoka Uruguy. Nafasi
ya Naibu Mkurugenzi Mkuu iliyokuwa na ushindani mkubwa kati ya
Mmarekani Denis Delehantty na Mswiss Pascal-Thienry Clivaz ambapo Clivaz
alishinda nafasi hiyo.
Ujumbe wa
Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mh.
Prof. Makame Mbarawa wakifurahia ushindi wa Tanzania kuchaguliwa katika
Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Duniani leo. Tanzania imekuwa
miongoni mwa nchi 40 zinazounda Baraza hilo, Kati ya nchi wanachama 192
Post a Comment