Mkuu wa Jeshi la
Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Raphael Muhuga aliyemwakilisha Mkuu wa Majeshi
ya Tanzania katika sherehe za maadhimisho ya miaka 67 ya Umoja wa Mataifa tangu
kuzaliwa kwake
Mgeni rasmi Waziri wa
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samwel Sitta akiwasili katika viwanja vya
Karimjee jijini Dar es Salaam leo katika Kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Umoja
wa Mataifa Tanzania kusheherekea miaka 67 tangu uanzishwe
Mratibu Mkazi wa Umoja
wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou akimlaki na kumtambulisha kwa wakurugenzi
wa UN Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samwel Sitta kwenye viwanja
vya Karimjee jijini Dar es Salaa leo
Waziri wa Ushirikiano
wa Afrika Mashariki Samwel Sitta akizungumza katika sherehe za kutimiza miaka 67
tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa (UN) katika viwanja vya Karimjee jijini
Dar es Salaam, Sitta aliipongeza Umoja wa Mataifa kwa kuisaidia Tanzania katika
nyanja mbalimbali za maendeleo ili kutokomeza umaskini.Waziri Sitta alisisitiza
kwamba bado Umoja wa Mataifa unakabiliwa na changamoto nchini kama vile amani na
usalama, tatizo la njaa, mabadiliko ya tabia nchi na uwepo wa silaha za
maangamizi.Mh. Sitta alifafanua katika kilele cha sherehe hizo umuhimu wa
kupitia na kusaidia nchi zinazoendelea kufikia malengo ya millennia
Mratibu Mkazi
wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou akitoa nasaha zake wakati wa
maadhimisho ya umoja huo katika viwanja vya Karimjee alisema matatizo ya njaa,
kupanda kwa bei za mafuta na mtikisiko wa uchumi duniani ni kati ya changamoto
kubwa ambazo Umoja wa Mataifa inakabiliana navyo katika dunia ya leo. Dtk Kacou
pia aliipongeza Tanzania katika juhudi zake za kupunguza vifo vya wakinamama
wakati wa kujifungua na watoto ili waweze kufikia malengo ya millennia
itakapofika 2015.Mratibu Mkazi wa UN alisema Tanzania imepunguza kwa kiasi
kikubwa maambukizi mapya ya ugonjwa wa Ukimwi







Post a Comment