Mkurugenzi Mkazi
wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot
akielezea jinsi shirika hilo linavyoshirikiana na serikali ya Tanzania katika
kufanikisha miradi mbali mbali ya maendeleo katika kuhakikisha nchi inapiga
hatua kwenye kukuza uchumi. Kulia ni Mwandishi wa Radio France International
(RFI Kiswahili) Bw. Ali Bilali.
*****************************
Umoja wa Mataifa umeanza
kuadhimisha wiki mahsusi kwa ajili ya Umoja huo kwa kufanya shughuli mbalimbali
ambapo nchini Tanzania taasisi za Umoja wa Mataifa, Serikali ya Tanzania na
mashirika ya kiraia wanakutana kuzungumzia maswala mbalimbali yahusuyo
maendeleo, utawala bora na njia za kupiga vita umaskini
uliokithiri.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa
shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Maendeleo nchini Tanzania UNDP
Philippe Poinsot, amesema Tanzania ni nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa ambayo
inawajibika vizuri kwenye umoja huo.
Mbali na hayo Mkurugenzi
huyo wa UNDP amesema kuwa Umoja wa Mataifa unachangia kwa kiasi kikubwa
kupunguza umasikini uliokithiri nchini Tanzania ambapo takriban dola za Marekani
lakini nne milioni hutolewa katika kipindi cha miaka
minne.
Wiki ya umoja wa mataifa
imeanza kuadhishwa Oktoba 17 na itafikia kilele Oktoba 24 mwaka huu.
Post a Comment